MADWANI MPWAPWA WALIA NA SHERIA ZA MADINI.


BARAZA la madiwani katika halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa limeiomba ofisi ya ofisa madini mkazi Dodoma  kuweza kuwajengea uwezo madiwani hao  na wadau wanaofanya kazi za madini  katika halmashauri hiyo  ikiwa ni mkakati wa kukuza mapato ya ndani ya halmasahauri hiyo.
Akisoma taarifa  ya utekelezaji  wa kamati ya fedha  uongozi  na mipango katika kipindi cha  mwezi julai  hadi septemba 2017 diwani wa kata ya Lumuma bwana Jocktan Cheliga amesema kuwa pamoja na  wilaya ya Mpwapwa kuzungukwa na neema ya madini ya aina tofauti tofauti  lakini wameshidwa kufaidika na rasilimali hiyo kutokana na madiwani wengi kuto kujua taratibu za upatikanaji wa mirahaba  ya madini katika maeneo husika.


Diwani wa kata ya Mazae bwana wiliamu Vahae akichangia mjadala katika kikao cha madiwani Mpwapwa.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana Donart Ngwezi amesema kuwa lazima kuwepo  na ushirikiano  wa pamoja  kati  ya ofisa madini mkazi  wa Dodoma kuweza kuwapa semina juu ya kuweza kusimamia  mapato yatokanayo na madini katika halmashauri yake ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya wilaya hiyo kukuza  mapato ya ndani.
Kwa upande wake kaimu ofisa madini mkoa wa Dodoma na mjiolojia na mtafafiti wa miamba na madini bwana Joshua Nduche amesema ofisi yao iko tayari kuwapitisha  katika sheria mbalimbali zinaozo ongoza shughuli za madini hapa nchini.

mbunge wa MPwapwa George Lubeleje.
Aidha bwana Nduche amewashauri madiwani wa halmasahauri hiyo kuweza kutunga sheria ndogo ndogo za halmashauri ili kuweza kukusanya mapato  katika madini mengi yanayopatikana katika wilaya hiyo.
Mmoja wa madiwani  kutoka katika kata ya Mazae Bwana Wiliiam Vahae amesema  miaka mitano iliyopita  Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya iliosifika kwa kutoa madini  ya Rubi ya kiwango cha juu Afrika  Lakini wilaya hiyo hakunufaika  na chochote  na kubaki kuwa maskini na kuachiwa mashimo  na uharibifu wa mazingira.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.