Kigoma Kusini, David Kafulila ameilipua Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) kuwa imekithiri kwa rushwa. Kutokana na tuhuma hizo, Kafulila amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuvunja kamati hiyo, vinginevyo yeye atajiondoa. Pia mbunge huyo ameitaka Kamati ya Maadili kulitumia Bunge kumvua ubunge, Badwel, kutokana na tuhuma za kupokea rushwa zinazomkabili. Kafulila alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa, wananchi hawatakuwa na imani tena na kamati hiyo. “Ikumbukwe Juni 13, 2011 nilieleza bungeni namna wabunge wa Kamati ya LAAC wanavyoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, huku nikimtaja kwa jina Mbunge wa Bahi, Omary Badwel kuwa ni miongoni mwao,” alisema Kafulila ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo. Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi ya Takukuru, Alex Mfungo alisema juzi kuwa mbunge huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo. Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema hana taarifa zozote za mbun...