WANANCHI WATAKA KUELIMISHWA KABLA YA MAONI YA KATIBA.
Na Noel Stephen -mpwapwa 19,05,2012
Wanachi jimbo la kibakwe wialayani mpwapwa wameomba swala la ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika mchako wakatiba lazima upewe kipaumbele ili kuweza kupata katiba yenye matakwa ya weanachi wote hapa nchini.
Wito huo umetolewa jana na wananchi wa jimbo la kibakwe wilayanoi mpwapwa katika mdahalo wa katiba ulio fanyika katika ukumbi wa muleba , na uliandaliwa na mtandao wa mashiriaka yasiyo kuwa ya kiserikali wilayani mpwapwa NGOMNET(Non governmental oganazationMpwapwa nert work)
Wakitoa maoni yao katika mdahalo huo wananchi hao walisema kuwa mchakato wa kuwa na katiba mpya ni mkubwa na tena umechelewa mno hivyo vingozi wanatakiwa kutoa kwanza elimu ya uraia kuhusu haki ya binadamu na katiba ya nchi ili kujenga Taifa lenye kuwajibika na kujua haki na wajibu wao kwa serikali yao na haki zao za msingi.
Akiongea nmmoja wa wachangiaji ambae ni diwanmi viti maluumau Bi Pamela Mnemele alisema kuwa elimu ya uraia juu ya katiba ni ni dai la msingi ili kuweza kuleta ushirikishwaji mpana wa wananchi katika kujadili mambo muhimu ya kimaendeleo katika katika maeneo yao hususani mambo ya ardhi na kilimo chenye tija tanzani kwa kumjali mkulima mdogo wa pembezoni.
Aidha akiongea juu ya muungano wa Tanzania na Zanzibar mwalimu Kelvin Haule alisema kuwa mchakato wa katiba uwe ni fulsa ya tiba (mwarobaini) kwenye suala muungano wa Tanzania .
Pia walisema kuwa katiba ya sasa tanggu uhuru imebadilishwa mala kumi na na nne bila kuwahusisha wananchi ambao ni ndio walipaswa kubadilisha katiba hiyo.
Hivyo walidaia kuwa katiba mpya itakapo patikana isibadilishwe kipengele chochote mpaka kuwepo na ridhaa ya wanachi wote tofauti na katiba ya sasa aliyo kuwa ikibadilishwa kwa maslahi ya chama tawala au kuwabeba baadhi ya vingozi wa ganzi ya juu serkalini.
Akiwasilisha mada ya dhana ya katiba Bwana ENOCK KIJO kutoka jukwaa la katiba nchini alisema kuwa katiba ndio huitoa mstakabali wanchi njisi inavyo takiwa iwe ,na ijingozeje, na mamlaka ya kuongoza nchi hutoka mikon I wa wananchi na sio mikanoni mwa wananchi.
Alisema kuwa katiba ili iweze kuwa katiaba lazima iwe na misingi mikuu mitanoa ambayo aliisema kuwa nilazima iandikwe na wananchi na sio kundi dogo la wananchi kama ilivyo fanya katika katiba tuliyo kuwa nayao ambayo alisema kuwa iliandikwa na wananchi ishirini ikiongozwana mzee Thabit kombo na PIUS MSEKWA akiwa akitibu wake..
Tena mchakato wa katiba lazima uwe na mafanano wa pekee wa nchi husika.
Comments
Post a Comment