MKUU WA POLISI ANATAKA AMANI ZANZIBAR
0digg
Elias Msuya na Salma Said, ZanzibarMKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mohamed Aboud pamoja na viongozi wa dini jana walitembelea maeneo yaliyoshambuliwa katika vurugu zilizotokea visiwani hapa.Ziara hiyo imekuja wakati hali ya amani ikielezwa kurejea visiwani hapa baada ya ghasia zilizoanza Jumamosi usiku na kuendelea hadi juzi.
Wakizungumza baada ya ziara hiyo, viongozi wa makanisa visiwani hapa walitoa malalamiko yao kuhusu vitendo vya uchomaji na uharibifu wa makanisa huku wakiitaka Serikali kutumia nguvu ya ziada kuingilia kati suala hilo wakisema tangu mwaka 2001 hadi sasa jumla ya makanisa 23 yameshachomwa moto Zanzibar.
Katibu wa Umoja wa Wachungaji wa Zanzibar, Jeremiah Ko
Comments
Post a Comment