MOVEMENT ZA CHADEMA HATARI KWA CHAMA TAWALA

0digg
Elias Msuya
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezindua harakati za mabadiliko hivi karibuni jijini Dar es Salaam unaojulikana kama ‘Movement for change’ (M4C)’ wenye lengo la kuchukua nchini mwaka 2015.

Katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Jangwani, viongozi wa Chadema wamefafanua maana ya harakati hizo, wakisisitiza kuingia Ikulu 2015.

Akizungumzia kampeni hiyo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema kuwa kuna gharama kubwa kuiondoa CCM madarakani.

“Kila mwananchi anawajibu wa kubadilisha maisha yake. Kila mtu anapaswa kuwa wakala wa mabadiliko. Kuiondoa CCM kuna gharama kubwa, kule Arumeru walichanga thumni zao na kila walichokuwa nacho na hatimaye tulishinda, au siyo? Tusije tukapata viongozi kwa fedha chafu” amesema Mbowe.

Ili kuhakikisha kuwa chama hicho hakiingiliwi na mamluki, Mbowe pia amesisitiza kuwa watakuwa makini na wanachama wapya wanaohamia Chadema akisema kuwa watatakaswa kwanza kabla ya kupewa uanachama.

“Kuna watu wamekuwa wakisema kuwa eti tunachukua wasaliti wa chama. Ngoja niwaambie, tutakuwa makini na kila mtu anayehamia Chadema na tutafanya kama Mungu, kwanza tutawatakasa na kuwasamehe” amesisitiza Mbowe.

Ameongeza kuwa chama hicho kimejengwa kwa zaidi ya miaka 20 na kimeweza kujenga ngome katika mikoa mbalimbali ya  Tanzania.

Kuhusu vitisho vya jeshi la Polisi Mbowe huku akinukuu kauli ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliyoitoia miaka ya 1960, amelitaka Jeshi hilo kutowati

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.