SERIKALI YAHITAJIKA KUPUNGUZA UTEGEMEZI
NA NOEL STEPHEN MPWAPWA
Imebainishwa kuwa serikali bado haiko makini katika kulifikia lengo la sita la mileniamu katika swala zima la kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu na Ukimwi kwa kuendelea kutegemea misaada kutoka serikali ya watu wa kimarekani.
Hayo yameibuliwa na wajumbe wa mkutano wa kamati ya kuratibu shughuli za huduma shirikishi za kifua kikuu na na ukimwi Wilayani mpwapwa mkoani Dodoma kwenye kikao cha kutadhimini huduma hizo hapa wilayani kilicho fanyika katika ukumbi wa Afya jana.
Akieleza mmmoja wa wajumbe alisema katika TANZANIA lazima itambue kuwa umakini wa utawala bora na uwajibikaji ni kutekeleza malengo waliyo jiwekea au waliyo iridhia katika mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo kutekeleza malengo ya mileniamu likiwepo lengo la sita la kupambana na kifua kikukuu, UKIMWI, na Malaria ili kuweza kuimarisha maisha bora na utawishaji wa jamii.
Aidha alidai kuwa “haiwezekani tunapo karibia kumaliza au kufikia mwisho wa muda wa malengo ya mileniamu bado SERIKALI YA Tanzania inategemea fedha za kuendesha mipango shirikishi ya kifua kikuu na ukimwi inategemea ufadhili wa mfuko wa maendeleo ya wamarekan(Glob fund) bila serikali yetu kuweka mikakati ya kuweza kulikabili tatizo hili kama ni tatizo la watanzania na walishughulikie wao wenyewe kwa kulitengea bajeti katika mipango yao ya halmashauri ya ili kuweza kuondoa hali ya utegemezi wa moja kwa moja kutoka kwa nchi wahisani”.
Akiongea mwenyekiti wa kikao hicho kaimu mganga mkuu wa wilaya DR.Pathan Mohamed alisema kuwa ni vyema halmashauri zetu kuingiza mpango huu kwenye bajeti za halimashauri ili kuweza kulimudu tatizo hili na kulitokemeza kabisa ifikapo 2015 kama maliengo ya mileniamu yanavyo taka.
Akitoa taarifa utekekelezaji mratibu wa shughuli za huduma za kifua kikuu na UKIMWI Dr JASTINI NYONI alisema kuwa kuanzia januari 2011-Desemba 2011 aliweza kupima wagojwa wa kifua kikuu wapatao wagojwa 191 wakiwemo wanaume 135 na wanawake 56, na walipima virusi vya UKIMWI walikuwa wanawake 55 na wanaume 125, ambapo walio kutwa na Virusi vya Ukimwi ni watu 79 wakiwemo wanawake25 na wanaume 54 amabapo alisema kuwa sawa na asilimia 30% ya wagonjwa walio sajiliwa kwa mwaka jana.
Pia Dr Nyoni alisema kuwa kwa mwaka 2012 wamepokea fedha zipatazo milioni33,895,231/= amabazo zitatumika katika kutoa huduma za upimaji wa makohozi katika vituo vya fya vinavyo toa huduma hii kwa sasa ili waweze kuboresha huduma hizo.
Tena wadau hao waliweza kutoa wito kwa wana siasa kuto ingilia kazi za kiutendaji ili kuweza kuleta tija katika huduma shirikishi za mapambano dhidi ya ukimwi na kifua kikuu kwa kuacha tabia ya kuwakataza wagonjwa kuto changia mfuko wa afya wa wilaya.(CHF)
Comments
Post a Comment