MADIWANI WATAKIWA KUWAJIBIKA
Na siyena Mbuta Mpwapwa
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wametakiwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na tamisemi.
Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa itafanikiwa kwa kiwango kikubwa endapo madiwani watapata mafunzo elekezi ili kutambua wajibu wao kikamilifu na hivyo kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria.
Kupitia mafunzo haya elekezi mliyoletewa na Tamisemi yatazaa matunda endapo mtayazingatia kikamilifu ili kuwa tatulia kero wananchi
Lengo la kutoa mafunzo kwa madiwani ni kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya kila siku pamoja na kujua sera ya utawala bora na uwajibikaji
Alisema Nchimbi iwapo diwani atatambua majukumu yake itamjengea ujasiri wa kutatua kero za wananchi wake kwa kutoa kipaumbele katika masuala ya afya, zahanati, shule na maji.
|
|
Kuwepo kwa mafunzo hayo itawasaidia madiwani kutambua majukumu yao na hivyo kushirikiana vyema na Halmashauri kiutendaji katika kutatua kero zilizopo ndani ya Wilaya.
Mfunzo hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma rasmi jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Comments
Post a Comment