MILIONI 850 ZATOLEWA MKOPO NA SACCOS YA MSHIKAMANO MPWAPWA
Na Noel Stephen Mpwapwa
Jumla ya shilingi milioni 815,000.000/zimetolewa kwa wananachama wapatao 800 wa Chama cha Ushirika Akiba na mikopo Saccos ya Mshikamano Baraza cha Mjini MPWAPWA.
Hayo yamebainishwa na meneja wa wa Saccos hiyo Bi YOKEBEDY PANGAWE alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake.
Bi Pangawe alisema kuwa chama hicho tangu kianzishwe mwaka 2003 hakijaweza kutoa mikopo ya kiasi kikubwa namana hiyo kwa wanachama wake ambapo wanachama hao wameweza kubadilisha maisha na kuongeza kipato cha familia na jamii inayo wazunguka ,
Aidha Bi Pangawe aliongezea kuwa mikopo iliyo tolewa ni kwa wanachama hao ni mkopo ya kilimo ambayo inaghrimu kiasi cha shilingi milioni 350,000,000/ na mikopo ya bishara ni milioni 450,000,000/ na mikopo ya dharula ilitolewa mikpo ya kiasi cha shilingi milioni 15,000,000/-.
Pia Bi Pangawe alisema kuwa mbali na kutoa mikopo hiyo kwa wanachama wake lakini wapo baadhi ya wanachama kuto kuitumia mikopo waliyo iomba kwa malengo yaleyale na kuhamisha matumizi ya mkopo kitu alicho kisema kuwa kina wapelekea kuingia matatani na mteja wakati wa ulipaji.
Na alidai kuwa wanachama wajenge moyo wa kusoma mikataba kabla ya kujaza fomu ya mikopo ili waweze kuelewa taratibu na kanuni za mikopo ili kupunguza mikwaruzano wakati wa malejesho ukifika au kwa mteja akishidwa kulejesha au anapo chukuliwa dhamana zake.
Tena Bi Pangawe aliwataka akina mama wengi waweze kujitokeza katika kuomba mikopo amabapo alisema kuwa kwa sasa idadi kubwa ya wanao chukua mikopo mikubwa n ni wanaume tofauti na akina mama ambao wao huchukua mikopo ya biashara ndogondogo ambazo haziwaletei tija akina mama wengi hapa nchini.
Alisema kuwa kwa sasa chama hicho kina wanachama wapatao 1483 na chama hicho kwa sasa kinauwezo wa kutoa mkopo wa shilingi milioni 8,000,000/ kwa mala moja kwa mwana chama tofauti na hapo awali amabapo walikuwa na uwezo wa kutoa shilingi 200,000/ laki mbili tu kwa mwanachma anae omba mkopo.
Comments
Post a Comment