VIONGOZI WA MOGADISHO WAJADILI MPANGO MKAKATI.

ala wa mpito

Na Mahmoud Mohammed, Mogadishu

Mei 30, 2012
Wachambuzi wa masuala ya siasa wameyakaribisha makubaliano yaliyosainiwa wiki iliyopita mjini Addis Ababa na viongozi wa Somalia, wakiyaelezea kama hatua inayotoa matumaini na kuonyesha kuwa nchi hiyo iko karibu kufungua zama mpya.
  • Wabunge wa Bunge la mpito la Somalia wakiandika dondoo wakati wa sherehe za kuapishwa mwaka 2004. Baada ya miaka 12, Somalia itakuwa na bunge lake jipya lililo rasmi baada ya kuisha kwa kipindi cha mpito mwezi Agosti mwaka huu. [Picha na Simon Maina/AFP] Wabunge wa Bunge la mpito la Somalia wakiandika dondoo wakati wa sherehe za kuapishwa mwaka 2004. Baada ya miaka 12, Somalia itakuwa na bunge lake jipya lililo rasmi baada ya kuisha kwa kipindi cha mpito mwezi Agosti mwaka huu. [Picha na Simon Maina/AFP]
Baada ya siku tatu za majadiliano ya ina kwenye mji mkuu wa Ethiopia kufungua zama mpya, viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini Somalia wamekubaliana ratiba iliyoandaliwa ambayo inayoelezea kwa kina hatua zinazotakiwa kufuatwa kumaliza kipindi cha utawala wa mpito na kuchaguliwa kwa Rais mpya.
"Makubaliano ya Addis Ababa ni alama yenye kutia moyo kwamba viongozi wa Somalia wamedhamiria kumaliza kipindi cha utawala wa mpito ndani ya muda uliopangwa na kuitoa nchi kutoka kwenye historia ya zama za mpito," alisema mchambuzi wa masuala ya siasa Abdullah Mahmoud, akisisitiza juu ya umuhimu wa viongozi hao kufikia muafaka bila ya shinikizo kutoka kwa wafadhili wa kimataifa na washirika wa nchi hiyo.
"Kuna tumaini la kweli kuwa Somalia inaelekea kwenye kwenye zama mpya za uhalali na utawala wa kidemokrasia, na jambo hilo litatoa fursa ya kufikia mwisho wa mizozo ya kisiasa na kero zake ambazo kwa kipindi kirefu zimekuwa zikiiandama nchi hiyo," aliiambia Sabahi.
Makubaliano hayo yalitiwa siani na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali, Spika wa bunge Sharif Hassan Sheikh Aadan, Rais wa Puntland Abdirahman Mohammed Faroole, Gavana wa Galmudug Ahmed Mohammed Alin, na mwakilishi wa Ahlu Sunna wal-Jamaa, Abdiqadir Mu'alim Noor.
Waliohudhuria kwenye adhimisho hiyo ni pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kimaendeleo (IGAD).
Washiriki wametoa wito kwa wafadhili na Jumuiya za Kimataifa kuchangia vifaa na msaada wa kifedha vitakavyowezesha kufanikiwa kwa mchakato huo. Wamesisitiza kwamba watu wa Somalia na Jumuiya ya Kimataifa hawatavumilia vikwazo kusitishwa ama vikwazo vyovyote dhidi ya mafanikio ya mpango huo, na kuahidi kumfichua yeyote atakayejaribu kuukwamisha na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake au dhidi yao.
Viongozi hao wamezitia moyo jumuiya mbalimbali ikiwemo Umoja wa Afrika, IGAD, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Taasisi ya Mikutano ya Kiislamu na kuziomba kuendelea kuunga mkono mchakato huo. Wametoa shukrani zao kwa jumuiya hizo pamoja na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa -- hususani Ofisi ya Siasa ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia -- kwa msaada katika mchakato huo.
Mhadhiri na mchambuzi wa masuala ya siasa Ahmed Abdiaziz pia amepongeza mafanikio hayo yaliyoletwa na wanasiasa nchini Somalia. "Mkubaliano ya Addis Ababa yameonesha kiwango cha ukomavu wa wanasiasa wa Somalia," aliiambia Sabahi. "Kwa mara nyingine wamethibitisha dhamira yao ya kumaliza kipindi cha mpito. Wameondoa pia vikwazo vilivyokuwa vinaukwamisha mchakato huo na pengine vingesababisha kutokutekeleza Mpango Mkuu na upokeaji wa katiba mpya."
Makubaliano yaliyofikiwa yametatua mzozo uliokuwepo hapo awali juu ya katiba mpya na uchaguzi wa wabunge, alisema Abdiaziz.
"Kutokana na ufinyu wa muda baina ya sasa na tarehe iliyopangwa kutekelezwa mpango huo mwezi Agosti mwaka huu, wanasiasa wanatakiwa kuusimamia kwa karibu mchakato huu, kudumisha mawasiliano na mahusiano na watu wa pamoja na wadau muhimu kwenye machakato huo ili kuweza kuufanikisha kwa urahisi," alisema.

Marekebisho katika makubaliano ya Garowe na Galkayo

Makubaliano ya Addis Ababa yamerekebisha Kanuni za Garowe na Makubaliano ya Galkayo na kuondoa vikwazo kwa kuupa nguvu Mpango Mkuu, kwa mujibu wa azimio la mwisho. Makubaliano hayo mapya yanarahisisha kasi ya utaratibu wa kuchagua wajumbe wa Bunge la Katiba, yanaweka baraza la upatanishi la viongozi wa kikabila na kuanzisha kamati ya kifundi kuwasaidia viongozi hao kutatua mizozo.
Baraza la upatanishi lenye wajumbe 25 ambao ni viongozi wa makabila – watano kwa kila kabila – litatatuwa migogoro inayoweza kuzuka wakati wa kuchagua wajumbe wa Bunge la Katiba, ambalo litapitisha katiba mpya.
Viongozi pia walikubaliana kuanzisha kamati ya kifundi kuhakikisha kuwa wagombea wa nafasi katika Bunge la Katiba na wajumbe wa bunge jipya wanafikia viwango vilivyoelezwa na Mpango Mkuu na Kanuni za Garowe.
Kamati hii ya kifundi vilevile itawasaidia viongozi wa makabila kutatua tofauti na kutatua migogoro baina ya makabila. Kamati hii ya kifundi itakuwa na wajumbe 36, kati yao 27 wakiwa Wasomali, wawakilishi wawili wa Ofisi ya Siasa ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia na wachunguzi saba wa kimataifa. Wasomali hao 27 watachaguliwa kulingana na muundo wa 4.5 na wadhamini wa mpango wa amani wamepewa jukumu la kuchagua wajumbe wa kamati hiyo ya kifundi.
Viongozi pia walikubaliana kuanzisha ofisi ya kuratibu ofisi mjini Mogadishu kufuatilia na kusimamia mawasiliano baina ya pande zinazoshiriki kwenye utaratibu wa mchakato.

Ratiba kwa hatua zilizobakia

Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya hivi karibuni, kamati ya kifundi lazima imalize kazi ya kuchagua wajumbe wa Bunge la Katiba kufikia tarehe 20 Juni, na wajumbe walioteuliwa kuwasili mjini Mogadishu kufikia tarehe 30 Juni.
Mkutano wa Bunge la Katiba utafanyika tarehe 2 Julai na limepewa jukumu la kupitisha katiba mpya tarehe 10 Julai.
Viongozi pia walikubaliana kuunda bunge jipya la shirikisho lenye wajumbe 225, nusu ya bunge la mpito. Wajumbe wa bunge jipya la shirikisho watachaguliwa tarehe 15 Julai, kuapishwa tarehe 20 Julai. Tarehe 4 Agosti, wabunge wa bunge hilo watamchagua spika na manaibu wake wawili.
Uchaguzi wa raisi utafanyika tarehe 20 Agosti 2012 na kukihitimisha rasmi kipindi cha serikali ya mpito.
Unaonaje kuhusu makala hii?

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Unaonaje kuhusu makala hii?

Maoni ya msomaji

( Sera za kutoa Maoni )
*Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Button

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.