SEHEMU ZA KIHISTORIA ZATELEKEZWA MPWAPWA

 N a Stephen Noel  Mpwapwa/

  Imegundilika kuwa japo kuwa Mji Mpwapwa una  maeneo mengi ya  kihitoria  na rasilimali za kale zilizoachwa na  Waarabu na Wajerumani lakini  rasilimali hizo bado hazija endelezwa ili kuweza kuisaidia Wilaya hiyo  Kiuchumi ,Kijamii  na Kisiasa,

Hali hiyo imegunduliwa na Mwandishi wetu wilayani hapo alipo fanya uchunguzi wa awali kutambua  maeneo hayo na rasilimali hizo zilivyo weza kuisaidia jamii ya Mpwapwa kijamii, kiuchumi na kisiasa.

 Alipo tembelea  maeneo hayo yaliyotumiwa na  wareno, waarabu,waingeleza na wajurumani ambao waligundua  kuwa mpwapwa kulikuwa ni  tawi la  njia kuu ya watumwa ya kati aliyo tumia  waarabu katika kuwasafirisha watumwa kutoka  Urambo-Tabora , Mpwapwa –Dodoma ,Kilosa –morogoro na  Chalinze Pwani hadi Bagamoyo.

Aidha kuna sehemu kama ya kisima walichokunywa maji watumwa na mabwana wao katika eneo la stendi ya Mpwapwa mjini wakiwa njiani kutoka Kigoma kuelekea Bagamoyo.

Pia kuna Mti wa Mlumbulumbu ambapo palichomwa Makanisa na Mfanyabiashara ya watumwa mwarabu ABUSHIRI kwa vile walikuwa wana pinga Biashara ya watumwa mwaka (1890) katika eneo la Vingh’awe palipojengwa Kanisa la watakatifu wote kanisa la Kiangilikana.

Tena katika Mti wa (Ficus) eneo la stendi ya mabasi Mpwapwa mjini ambao ulitumiwa na watumwa na Mabwana wao kupumzika baada ya safari ndefu kutoka Kigoma kuelekea Bagamoyo, vile vile njia waliyopitia ni eneo la Vingh’awe hadi stendi ya mabasi Mpwapwa mjini watumwa na mabwana wao.

 Akiongea na waandishi wa habari ofisi kwake bwana Amani Bendera  afisa muhifadhi wa mambo ya kale alikili kuto yaendeleza maeneo hayo kwa kisingizio cha ukosefu wa rasimali fedha kutokana na ufinyu wa bajeti na  wilaya kutokuona kuwa vyanzo hivyo vya kihistoria kuwa kipaumbele cha ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ya wilaya.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.