MAHAKAMA ZADAI KUINGILIWA NA SERIKALI KIUTENDAJI
Omana Gouth na Noel Stephen Mpwapwa
Imeelezwakuwa katika utendaji wa kazi wa Mahakama za Jamahuri wa Muungano wa Tanzania haziko huru kama inavyo ainishwa katika Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Hayo yamebainishwa na wajumbe wa mdahalo wa katiba uliofanyika katika Ukumbi wa ccm Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ulioendeshwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia NGOMNET Mpwapwa.
Akichanngia mada katika mdahalo huo mmoja wa washiriki Bwana JEMSI KAREIMAHA hakimu mfawidhi wa mahakama wa wilaya ya Mpwapwa alisema katika utendaji wa kazi katika mihimili mitatu ya dola ambayo ni Serikali,Bunge na Mahakama kunaonekana kuwa serikali inakuwa na madaraka makubwa kuzidi mihimili mingine katika utendaji kazi wake kutokana na muhimili mmoja kuutegemea muhimili wa mahakama kwa kuwezeshwa kifedha na vitendea kazi.
Aidha Bwana Kareimaha alidai kuwa katika utendaji wa kazi wa kutoa maamuzi ya kimahakama Rais anaweza kutengua hukumu iliyo iliyotolewa na hakimu au jaji kwa madaraka aliyokuwa nayo kikatiba kitu alichosema kinaleta utata wa kiutendaji.
Pia akiongezea mchangiaji mwingine bwana Kandido Mnemele mwakilishi wa kundi la walemavu wilayani mpwapwa (shivyawapwa) alisema kuwa katiba hiyo bado haifahamiki kwa wananchi wa vijijini na wala hawaijui rangi yake, na imeandikwa bila kuzingatia uhitaji wa makundi maluum kama walemavu wa macho,kwa kuandika katiba ya maandishi ya nukta nundu.
Bi ELLY MAKALA afisa wa Tasisi wa kuzuia na kupamabana na rushwa nchini PCCB alisema kuwa watanzania bila kubadilisha mtazamo wa kuwa na maadili na kufuata kanuni na sheria za kazi katiba mpya haiwezi kuwa jawabu la matatizo ya watanzania bila ya viongozi kuwa waadilifu.
“Hata tusemeje na tutunge sheria nyingi kiasi gani hatuwezi kutataua matatizo ya watanzania bila kubadilisha mtazamo wa viongozi kuwa waadilifu, jawabu la matatizo ya watanzani yamo mikononi mwao wenyewe kwa kujenga moyo wa kushiriki,kupanga na kufuatilia mipango ya kimaendeleo na kuwawajibisha viongozi wabadhilifu’’ Alisema bi makala.
Akitoa mada katika mdahalo huo mmoja wa wawezeshaji Daktari Sinda HUSSEN SINDA kutoka chuo kikuu cha Dodoma alisema kuwa TANZANIA haina Dira na dhima juu ya mstakabali wa Taifa juu ya siasa ujamaa na kujitegemea kuwa wanachi hawajui wanafuata siasa ya mlengo wa namna gani,kibepari,kibwenyenye,ua siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Comments
Post a Comment