WAJUMBE WA MKUTANO MKUU UWT WAAONYWA DODOMA.
WAJUMBE wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Dodoma wameaswa kuchagua viongozi makini na imara watakaokifanya chama kiendelee kuwa imara kutokana na mkoa huo kuwa makao makuu ya Chama. Pia amewataka wana CCM kupendana,kupunguza figisu,visasi,majungu,porojo na kuwa ili kufikia maengo ni lazima wanyanyuane na kuinuana kwa lngo la kumfanya kila mmoja atimize yale aliyoyapanga kwa msaada mkubwa wa mwanamke. Rai hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Dodoma Alhaj Kimbisa wakati akifungua mkutano huo ambapo amesema CCM nyumbani kwake ni Dodoma hivyo viongozi watakaochaguliwa lazima watambue hilo kwa kulinda heshima isipotee. Aidha amewaasa kutochagua viongozi wenye harufu ya rushwa bali wachague viongozi watakaokuwa wepesi wa kuwaunganisha akina na watakaoifanya jumuiya ijitegemee kiuchumi. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe 473 ambapo miongoni mwa nafasi zinazogombewa ni nafasi y...