SEHEMU ZA KIHISTORIA ZATELEKEZWA MPWAPWA
N a Stephen Noel Mpwapwa/ Imegundilika kuwa japo kuwa Mji Mpwapwa una maeneo mengi ya kihitoria na rasilimali za kale zilizoachwa na Waarabu na Wajerumani lakini rasilimali hizo bado hazija endelezwa ili kuweza kuisaidia Wilaya hiyo Kiuchumi ,Kijamii na Kisiasa, Hali hiyo imegunduliwa na Mwandishi wetu wilayani hapo alipo fanya uchunguzi wa awali kutambua maeneo hayo na rasilimali hizo zilivyo weza kuisaidia jamii ya Mpwapwa kijamii, kiuchumi na kisiasa. Alipo tembelea maeneo hayo yaliyotumiwa na wareno, waarabu,waingeleza na wajurumani ambao waligundua kuwa mpwapwa kulikuwa ni tawi la njia kuu ya watumwa ya kati aliyo tumia waarabu katika kuwasafirisha watumwa kutoka Urambo-Tabora , Mpwapwa –Dodoma ,Kilosa –morogoro na Chalinze Pwani hadi Bagamoyo. Aidha kuna sehemu kama ya kisima walichokunywa maji watumwa na mabwana wao katika eneo la stend...