WANANCHI WALALAMIKIA HUDUMA HAFIFU TANESCO MPWAPWA.
WANANCHI wa wilaya ya
Mpwapwa mkoani Dodoma wamelalamikia huduma duni na hafifu za
shirika la ugavi la umeme TANESCO wilayani hapa kuwa zinawarudisha nyuma
kimaendeleo
Wananchi hao
waliyoataoa malalamiko yao walipo kuwa wakiongea na mwandishi wa habari juu ya kuto ridhishwa na huduma zitolewazo na
shirika hilo kuwa zimekuwa za kusuasua na huchukua muda mrefu
kushughulikiwa kero zao kitu walicho
kisema kuwa kinachangia kudumaza uchumi
na maendeleo ya watu wa Mpwapwa.
Mmoja wa wananchi
wa wilaya hiyo bwana AHMAD UTAMU
alisema kumekuwa na ubabaishaji wa
ujazaji wa ramani pindi unaomba huduma za kuunganishiwa umeme ndani ya nyumba,kukatika katika kwa
umeme mara kwa mara kunakopelekea baadhi
ya watu kuunguza vitu vyao na kuwasababishia hasara kubwa.
Aidha bwana Ahmad alisema kuwa
shirika hilo limekuwa likikiuka mkataba wa huduma kwa mteja ambao
unalitaka kutoa taarifa kwa wateja wao pindi
umeme utapo katika na sababu zinazo
pelekea kukatika katika kwa umeme.
“Yaani kwa Mpwapwa
imekuwa tofauti yaani mvua kidogo tu
umeme umekatika na hawa watu wa Tanesco
hawatoi taarifa hadi siku tatu umeme unakatika bila taarifa huku wateja
tukibaki katika sintofahamu ya nini kinaendelea na ukirudi uanarudi kimyakimya
na kupelekea vitu vya watu kungua”aliongea Bwana Ahmad
Meneja wa shirika hilo
wilaya Mpwapwa Bwana BEATUS KEBWE amekili kuwepo kwa baadhi ya changamoto
zinazo ikabili ofisi yake kitu alicho sema changamoto hizo zinasababishwa
na uchache wa watumishi,vitendea
kazi na umbali na jografia ya
mpwapwa kunapelekea kuwapo kwa
malalamiko mengi ya wateja.
Aidha Kebwe alisema
kuwa “kwa wilaya yangu kijiji cha mwisho ninacho kihudumia ni umbali wa kilomita 150 kijiji cha
Malolo kwa hiyo tatizo likitokea kule
ni ngumu kuliatend kwa wakati kwa kuzingati hatuna magari ya kutosha lakini pia hata watumishi”alifafanua bwana
Kebwe.
Hata hivyo meneja huyo
alisema ili kuweza kupunguza changamoto
hizo shirika la Tanesco wialayani hapo limekusudia kuanzisha
Dawati la huduma ambalo itakuwa ni madwati yatakayo kuwa yanapatika
karibu na wateja huko kijiji kila kata lazima kutakuwa na
dawati la huduma.
Pia alisema wanampango wa kupanua huduma kwa wateja kwa
kufungua ofisi zingine za Taneco
katika tarafa ya Kibakwe,kijiji cha
Chipogoro na kata ya kinusi lengo lake likiwa kusogeza huduma zaidi kwa
wananchi.
Comments
Post a Comment