NCHEMBA ALAANI VITENDO VYA KIHARIFU.




WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amelaani vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa vikitokea katika maene mbalimbali nchini ikiwemo mauaji,vitendo vya utekaji,kupigwa na kutishiwa risasi kwa baadhi ya viongozi,wananchi pamoja na wanasiasa vilivyofanywa katika kipindi cha mwaka 2017.

Kutokana na hayo Waziri Mwigulu ameitaka jamii katika mwaka 2018 kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya kiuhalifu.

Hata hivyo Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi inakutana na waandishi ili kueleza mipango mikakati ya kutokomeza vitendo vya uhalifu mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi mjini Dodoma,Waziri wa wizara hiyo Mwigulu Nchemba amesema kuwa ili kutokomeza vitendo vya kiuhalifu jamii inatakiwa kuwa mustari wa katika kutoa taarifa za wahalifu.

Waziri Mwigulu akazungumzia namna wizara kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ilivyojipanga kwa kipindi cha mwaka 2018 katika kudhibiti vitendo vya kiuhalifu vinavyofanywa na Baadhi ya watu wasio na nia njema

Kauli mbiu ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa kipindi cha mwaka 2018 ni zuia Uhalifu kabla haujatokea ikiwa na lengo kuu la ikiwa ni kuweka kipaumbele kwa raia yoyote kutoa taarifa za uhalifu kabla haujatokea.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.