KOROSHO MKOMBOZI WA UCHUMI KWA WAKULIMA MPWAPWA
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabiri Shekimweri akikagua kitalu cha Miche ya Korosho.
SERIKALI Wilayani
Mpwapwa mkoani Dodoma yawapa
changamoto wanaufaika wa wa Mpango wa kaya maskini TASAF
kuacha kutegemea fedha za ruzuku yawataka kujikita katika kilimo cha Korosho ili kuwa na uchumi endelevu.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir
Shekimweri juzi alipotembelea miradi uoteshwaji wa miti
na vitalu vya korosho ya wanufaika
wa Mpango wa katika vijiji
vya Idilo,Gulwe,Kingiti na Iyenge.
Shekimweri alisema wao
kama serikali lazima wawasaidie wanafaika wa mpango huo kuweza kuwa na uchumi endelevu kwa kujikita katika ulimaji
wa zao la korosho ambalo ndani ya miaka mitatu linaweza kubadilisha uchumi wa
mtu mmoja mmoja na kaya kwa ujumla kuliko kutegemea fedha hizo za
ruzuku ya kila mwezi ambazo
zitamsaidia kupunguza changamoto zake lakini si kuyamaliza.
“Sasa mpango huu wa kila mnufaika kulima heka mbili za zao la korosho zitasaidia sana wanufaika kuwa na uchumi endelevu hata kama mradi utakapo isha,kama serikali tunaamini mlegwa
huyu akilima korosho ndani ya miaka
mitatu huyo mtu si yule ambae alikuwa anategemea fedha za ruzuku uchumi wake lazima ubadilike”
aliongea Shekimweri.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa akifafanua baadhi ya madini yanayo patikana katika Bibo la korosho kuwa ni vitamin c kwa wingi.
“Kwa mfano sasa mtu anaepokea
kiasi kidogo sana ni shiringi elfu ishirini lakini akilima korosho korosho heka mbili tu
ana uhakika wa kupata kiasi cha shilingi milioni nae kila mwaka sasa hapo si wote tutakuwa matajiri tutakuza
uchumi wa kaya uchumi jamii na wilaya
kwa ujumla inawaomba wote tujiingize
katika kilimo hiki ambacho kitaleta mapinduzi makubwa sana ya kiuchumi na mazingira ndani ya wilaya ya
Mpwapwa” aliongea Zaidi Shekimweri.
Aidha mku wa wilaya hiyo
ametumia Fursa kuwakanya wale wanao pokea fedha za Tasaf na
kuzitumia nje ya Mpango kuwa lazima wazingatie masharti mpango
huo ili ziwanufaishe kwa kiwango
cha juu ili pindi mpango utakapo isha waweze kupima matokeo ya mradi huo.
Kwa upande wake mratibu wa Tassaf Wilaya ya Mpwapwa bwana Paskali Symlis alisema kuwa Mpango
huo wa kunusuru kaya Maskani
tangu uanzishwe mwaka 2014 kwenye
vijiji 57 kati ya vijiji113 vya wilaya
ya Mpwapwa ambapo
unanufaisha kaya 5990.
Bwana Jeremia alisema
hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu
mpango huo umeweza kutoa ruzuku kwa
awamu 20 na umla cha kiasi cha shilingi
billion 4,774,383,500/= zilitolewa kwa walegwa kama ruzuku ya msingi na
malipo kwa ajili ya ajila za muda.
Pia Bwana Jeremia alisema
ili kuhakikisha kuwa walegwa wanakuwa na kipato cha uhakika
na endelevu halmasahauri kwa
kushirikiana na walegwa kupitia
mpango wa umeanzisha kilimo cha korosho
kwa vijiji 22 vyenye walegwa 2396.
Alisema katika mpango huo wanategemea kulima heka 4792 za
korosho ambazo zitaweza kuleta
mabadiliko ya kijani pamoja na uchumi wa kaya na jamii kwa ujumla.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango
wa Mpango huo BiJaneth Yeremia alisema pamoja na mpango huo kuwalipa baadhi ya walegwa katika ajira za
muda lakini walegwa 12 wa kijiji cha kingiti hawakulipwa malipo yao
japo kuwa walifanya kazi.
Pia miongoni mwa
wanufaika wengine ambae hakauta jina lake kuandikwa alisema kuna baadhi ya watendaji na baadhi ya
wasimamizi wa mpango huo CMT wamekuwa wakiwakata fedha zao za ruzuku pasipo kuwa na maelezo ya kutosheleza kitu alicho kisema kuwa kinaonyesha mianya ya
rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Comments
Post a Comment