WALIMU MPWAPWA WAASWA KUTO KUKOPA MIKOPO YA KUWAZALILISHA.
Kaimu
ofisa Elimu sekondari wilya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bi Frola Mkwama
amewataka walimu kijishughulisha na miradi midogo midogo ya kujiongezea kipato
kuliko kujiingiza kwenye mikopo ya watu binafsi
ili kuepuka fedheha zinazo wapata pindi washidwapo kulipa.
Bi
Mkwama aliyasema hayo juzi katika mkutano mkuu wa kumi na tisa wa chama cha
kuweka na kukopa cha Mpwapwa Teachers Saccos iliofanyika katika ukumbi wa CCM
mjini hapa.
Bi
Mkwama alisema siku hizi kumeibuka maduka mengi yanayo kopesha na hivyo walimu wengi wamejikuta wakidaiwa kadi za Benk na
namba za siri kitu kinacho sababisha
walimu wengi kujikuta wakiishi maisha magumu.
Aidha
Bi Mkwama alisema “kwa mwalimu kuobwa
kadi na namba ya siri ni kinyume na sheria na privace ya mtu lakini pia haya
maduka yanayo kopesha sijui kama yamesajiliwa kama tasisi za kukopesha bali
yamesajiliwa kama maduka ya kuuza bidhaa hivyo hata watu wa biashara yachunguze
maduka hayo.
Pia
alisema hata riba ya maduka hayo iko juu
sana kiasi kwamba yanamuuza sana mkopaji
alisema ili kuweza kuondokana na hilo walimu lazima kujishughulisha na
miradi mingine ya kiamaendeleo kama ufugaji biashara ndogondogo ,kwa lengo la
kuepukana na mikopo ambayo si rafiki kwao.
Kwa
upade wake Mwenyekiti wa Chama hicho Bwana Piniel Loilole kwa mwaka 2017 jumla
ya shilingi mlion 99,940,000/= zilitolewa na chama hicho kwa wanachama 88 kwa kipindi cha januari –December 2017kama mikopo ya kawaida
na shilingi milioni 8,910,000 kama mikopo ya dharula.
Loilole
alisema kuwa wameamua kutoa mikopo hiyo
ili kuweza kuboresha ustawi wa mwalimu na kuweza kujiinua kiuchumi na kimaendeleo kwa lengo la kuodoka kwenye kipato cha chini
na kufikia kipato cha kati ambaocho kitaweza kumsaidia mwalimu, kuweza kujenga
nyumba bora ,kusomesha na kuwekeza kwenye miradi mbalimbali kama ya
kilimo, na ufugaji.
Kwa
upande wake meneja wa Saccos hiyo
Joakimu Mokiwa alisema kuwa mikopo hiyo italeta mabadiliko ya mwanachama mmommoja
na kukuza uchumi kwa kaya na taifa zima.
Pia
iliongeza kuwa pamoja na kuwezesha wanachama wake alisema kuna changamoto kubwa iliyowakabiri kwa mwaka2017 ni baadhi ya
watumishi waliogundulika kuwa na vyeti feki
kusimammishwa kazi na hivyo kupelekea chama hicho kupata hasara ya jumla ya shilingi milion 6,789,6650/=
Hata
hivyo alisema mwajiri kuchelewesha
makato ya walimu hao kuingia chamani na
kusabibisha mzunguko wa fedha chamani kusuasua katika uendelevu wake.
Aliongeza kuwa
walimu lazima waachane na tabia
ya kuchukua mikopo na kufanyia malengo
ambayo hayakuombewa kwenye mkopo
aliwataka kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati.
Pia Mmoja wa wanachama wa Sassos hivyo mwalimu
Neema Mbise alisema wanajikuta
wakijiingiza kwenye maduka ya wakopeshaji yasiyo sajiliwa kutoka na
mchakato wa Saccos hiyo kuwa mrefu zaidi hivyo ameuomba uongozi wa saccos hiyo
kuweza kupunguza masharti ya mkopo ili
mwalimu anifaike na fedha yake.
Comments
Post a Comment