MIMBA ZIMEKUWA KIKWAZO CHA ELIMU MPWAPWA.
Baadhi wa Wadau akisikiliza mjadala wa Elimu wilayani Mpwapwa.
MKUU wa mkoa wa Dodoma
Dkt Binilith Mahaenge amesema nchi zote zinazoendelea zinatakiwa kuwekeza kwenye Elimu ili kuweza
kufikia katika nchi zilizo endelea.
Dkt Mahenge alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua mkuno
wa wadau wa elimu wilayani Mpwapwa uliofanyika katika chuo cha ualimu mjini
hapa.
Mahenge alisema nchi zote zilizoendelea ziliwekeza nguvu kubwa katika elimu hadi kufikia maendeleo zinazojivunia kwa
sasa na kuwa na rasilimali watu
wengi na wazalishaji tofauti na nchi
zinazoendelea kundi kubwa limekuwa si la
kuzalisha na hivyo kubaki kama obwe
kubwa la kiuchumi.
Dkt Mahenge alisema kuwa “tunaweza kutoka katika nchi
zinazoendelea na kufikia nchi zilizo endelea
kwa kuwekeza sana sana katika elimu
tusione nchi zilizoendelea ziko mbali waliwekeza san asana kwenye
elimu ndugu zangu hatuwezi kufika popote
tukiendelea kufanya vibaya katika elimu
lazima tuwandae rasilimali watu ambao
watakuwa wazalishaji katika kilimo,huduma za jamii nk”aliongea Dkt Mahenge.
Katika mjadala huo ulioandalia na halmasahauri ya wilaya
yampwapwa ikiwa na lengo la kutadhimini
kubaini change moto, kupanga mikakati na ya
kuinua elimu katika wilaya
hiyo ambayo zaidi ya miaka mitatu mfululizo imekuwa
ikifanya vibaya katika matokeo ya darasa
la saba na kidato cha nne.
Kwa upande wake Mkuu
wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri alisema tataizo la mimba mashuleni limekuwa
kikwazo kikubwa cha watoto wa kike kuto fikia ndoto zao na kuachishwa masomo kabla ya kuhitimu darasa la saba au kidato cha nne.
Shakimweri alisema kwa mwaka 2017 jumla ya wanafunzi 69
walilipotiwa ujauzito wakiwa shueni na hivyo kuwapelekea kuachishwa
masomo kwa mujibu wa sera ya elimu na sheria ya elimu ya mwaka 2016.
Mkuu wa wilaya hiyo amewaomba wadau wa elimu wilaya hapo
kuweza kuchunguza kwa mapana na kubaini chanzo cha mimba mashuleni ili kuweza
kuokoa kikazi cha wasichana ambao hufifisha ndoto zao kabla ya muda.
Ofisa Elimu Msingi wilayani hapa Bi Mery Chakupewa alisema kwa mwaka 2017
iliweza kushika nafasi ya pili kimkoa ambayo ilifaulu kwa ufaulu wa asilimi 63.68
ambayo kitaifa ilishika nafasi ya 112.
Bi Chakupewa
alisema kuwa pamoja na kufanya
vizuri katika mtihani wa Darasa la saba
alisema wilaya hiyo inakabiliwa na chanagamoto kadhaa kama uhaba wa vyumba vya
madarasa,upungufu wa madawati, pamoja na miundo mbinu hafifu kwa baadhi ya maeneo kunako pelekea baadhi ya walimu
kukimbia maeneo hayo au kuacha kazi kabisa.
Akitaja shule 10 zilizofany vizuri kwa mtihani kuwa ni shule
ya msingi Mtejeta,Vighawe,Kikombo,,Pwaga,Mangangu, Mbunga,Kisisi,Mpwapwa,Kizi
na Isighu. Shule zilizo fanya vibaya kumi za mwisho alisema kuwa ni shule ya
msingi, Makutupa ,Nzugilo,Kilambo,Igoji Kusini,Idaho,Lufu,Msanga mbuya na
Gomuhungile ,
Comments
Post a Comment