SERIKALI YAJIPANGA KUTOA CHANJO YA SARATANI
Naibu waziri wa afya mandeleo ya jamii, jinsia,
wazee, na watoto Dr. Faustine Ndungulile amesema kuwa serikali inatarajia
kuanza kutoa chanjo ya kujikinga na saratani ya matiti pamoja na saratani ya
shingi ya kizazi kwa mabinti wenye umri wa miaka 14 mapema mwezi April mwaka
huu.
Kwa mujibu wa Takwimu za shirika la afya duniani
ya mwaka 2012 zinaonyesha kuwa 80 ya saratani ya mlango wa kizaza zinatokea
katika nchi zinazoendeleo,ukilinganisha na nchi nyingine za afrika mashariki
Tanzania inaongoza kwa kuwa na wagonjwa 50.9 kwa kila wanawake 100,000 lakini
pia tunaongoza kwa kuwa na vifo 37.5 kwa kika wanawake 100,000.
Akizungumza leo mjini hapa wakati akizindua
kampeni ya kupima saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti Dr. Ndungulile
alisema kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo serikali imeona ni vyema kuanza
kutoa chanjo wa ugonjwa huo.
Amesema kuwa watarajia ndani ya mwaka huu kutoa
chanjo kwa mabinti wapata 6,16,734 nchi
nzima.
Amesema kuwa wao kama serikali baada ya kuona
utafiti huo wameona wajielekeze kwenye kutoa chanjo hiyo ili kuwalinda mabinti
nakupunguza uwezekano wa wao kupata saratani ya mlango wa kizazi huku akisema
kuwa saratani hizo zinaweza kuepukika.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr.
Binilith Mahenge akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi amesema kuwa
maamuzi ya kutoa kampeni hiyo ni sahihi ili kufanya wananchi tumia fursa hiyo
kupima afya zao na badae kupataiwa matibabu.
katika chanjo hiyo wamelengwa mabinti ambao wapo
mashuleni hivyo wazizi wanaombwa pindi wapatapo taarifa hizo kutoka kwa waalimu
wa shule watoe shirikiano kwani maamuzi ya serikali ni mema kwa mabini hao.
Comments
Post a Comment