VITA YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI ZAIDI YA UGAIDI.
Hii ni miongoni mwa nyumba za mwanzo am[o baba wa taifa marehemu Nyererealikuwaakifanyia mikutano yake humo ikombioni kusomwa na maji kutokana na uharibifu wa maxingira.
VITA YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI ZAIDI UGAIDI.
MAZINGIRA ni uhai,Mazingira ni vitu vyote vinavyo tuzunguka vyenye na uhai na visivyo na uhai, vitu vyenye uhai ni mimea na wanyama na visivyo uhai ni pamoja na hewa ardhi na maji, mazigira yanahusisha vitu vyote kuendelea na kuwepo kwa viumbe vingine.
VITA YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI ZAIDI UGAIDI.
MAZINGIRA ni uhai,Mazingira ni vitu vyote vinavyo tuzunguka vyenye na uhai na visivyo na uhai, vitu vyenye uhai ni mimea na wanyama na visivyo uhai ni pamoja na hewa ardhi na maji, mazigira yanahusisha vitu vyote kuendelea na kuwepo kwa viumbe vingine.
Maisha ya viumbe
vilivyopo na vijavyo utegemea mawasiliano mazuri kati ya mazingira watu na,uhai, uhuru na usatawi wa taifa letu
la sasa hutegemea sana maisha yanayo tuzunguka, leo hii uharibifu wa mazingira
umekuwa ni nitishio kubwa la uhai wa
binadamu na mataifa mbalimbai ulimwenguni.
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tishio la usalama wa maisha
kama ilivyo kwa ugaidi na vita, sote tumekuwa mashaidi njisi tunavyoshuhudia
njisi mvua zimeendelea kushuka na kuto kuwa za kutabilika siku hadi
siku ,joto limezidi kuongezeka
ukubwa wake kutokana na uharibifu wa mazingira katika hali
hiyo ndicho miongoni mwa sababu kubwa za migogoro
ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima
,uhaba wa chakula, na umaskini iwapo hatua za makusudi za uhifadhi wa mazingira hazitachukuliwa vya kutosha.
Mazingira ni afya
yetu mazingira ni uhai wetu na mazingira ni uhuru wetu.
Katika nchi yetu ya Tanzania misitu alianza kuhifadhiwa
tangu enzi za ukoloni mwaka 1859 wakati wa enzi za wajerumani,juhudi hizo
ziliendelezwa na waingeleza mala baada ya
vita kuu ya dunia mwaka 1914-1918
baadhi ya misitu ilianza kutengwa na kuhifadhiwa kisheria mwaka 1930 -1952.
Kimsingi masuala ya
uhifadhi ilipewa kipaumbele sana
wakati wa serikali ya waingeleza ,wakati sera ya kwanza ya misitu
iliwekwa mwaka 1953 ,ilifanyiwa malejeo mwaka 1957 ambapo ilitumika hadi mwaka
1977, ambapo ndiyo iliopo hadi sasa, 1998 Sheria ya misitu namba 14 ya mwaka
2002 ilitayarishwa mahususi kwa lengo la
kuhifadhi na kuendeleza misitu kisheria.
Misitu ni mali asili inayo hifadhi maji kwa kiwango kikubwa
sana ikumbukwe kuwa mizizi ya miti
husababisha nyufa katika ardhi na kutokea kwa chemchem nyingi za asili.
Uharibifu wa mazingira na misitu una madhara makubwa kwa
uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja uihifadhi wa mazingira afya na mazingira pia
ni sehemu ya kawaida kwa maisha ya mwanadamu popote alipo.
Wilayani Mpwapwa, yako maeneo ambayo kihistoria yalikuwa ni
sehemu tegemeo kubwa kwa maisha ya watu ikiwa ni pamoja na Maendeleo yao. Upo
ukweli usiopingika kuwa Mpwapwa ilikuwa ikiongoza kwa kulisha chakula Mkoa
Mzima wa Dodoma pamoja na mikoa jirani, kabla ya kuharibika kwa mazingira
katika wilaya hiyo.
Hivi sasa imebaki historia kwani maeneo mengi yanaonekana kuharibika vibaya huku mamlaka husika zikiwa zinaumiza kichwa juu ya namna ya kukabiliana na uharibifu huo.
Kijiji cha Mima,Lwihomelo,na kijiji cha Kibodyani ni mfano wa maeneo ambayo yalikuwa na mazingira mazuri lakini kwa sasa ni miongoni mwa Vijiji vya mfano mbaya kwani Milima ya kijiji hicho hivi sasa imekuwa ni vipala.
Wananchi wamevamia maeneo ya milima na kuchoma moto, kulima katikati ya msitu lakini bado watendaji
wa kata, vijiji , na wanasiasa wanaendelea kupata kigugumizi njisi ya
kuwachukulia hatua waharifu wa mazingira hayo tunajiuliza ni kuto kuelewa
sheria au ndo ile hali ya kukingiana vifua.
Moja wapo ya Eneo lililofyekwa katika mlima Mkanana kata ya Berege Wilayani Mpwapwa.
Bila shaka wanashindwa kufanya hivyo kutokana na sababu zao binafsi ambazo wanazijua wao, ama ni kwa makusudi au hata kuaminishwa kuwa labda na wao ni miongoni mwa watu hao wanaoharibu mazingira wao wakishirikiana kwa uzembe.
Hata hivyo si vema kuhukumu kwa upande mmoja, lakini inafaa kutazamwa kwa mapana na marefu ili kubaini ni wapi panapohitaji kuangaliwa kwa macho mawili.
Salum Kabanda ni meneja wa wakala wa kuhifadhi misitu ya asili wilayani Mpwapwa ambaye anatahadharisha kuwa kama juhudi za makusudi hazitachukuliwa ni wazi kuwa wilaya hiyo muda mfupi ujao itakuwa ni jangwa.“Achilia mbali kugeuka jangwa, lakini katika kipindi cha miaka 10 ijayo hakutakuwa na maji katika wilaya hii kama mnavyoona hilo halifichiki nduguzangu,’’anasema Salum.
Kabanda anasema kuwa ifikapo mwaka 2027 hakutakuwa na maisha katika wilaya hiyo na kwamba viumbe hai wote wataishi kwa taabu na huenda vifo vikatawala kwani juhudi za kuharibu mazingira ni kubwa kulikojuhudi za kuyalinda.
Mtaalamu huyo anaonya kuwa hakuna sababu za aina yoyote kwa binadamu kupigalamli juu ya kwa nini maisha yanakuwa ni magumu wilayani Mpwapwa bali ni vema kuangalia wapi waliko jikwaa.
Kauli ya mtaalamu huyo zinamfanya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa JabirShekimweri kuapa kuwa atakufa na waharibu mazingira.
Mkuu huyo ambae tangu ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya mwaka mmoja uliopita anasema hana kitu kingine ambacho anasema kujivunia isipokuwa ni namna ambavyo atafanikisha mapambano na waharibifu mazingira Mpwapwa.
Anasema ili kufikia malengo lazima waanze kupanda miti katika tasisi za serikali kama shule za msingi,sekondari na tasisi zote za serikali pia ataongoza mashambulizi ya watu ambao watakuwa ni wakata miti na kuharibu vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kilimo cha milimani.“Nitatumia hata dola kwa ajili ya kuongoza mashambulizi ya mapambano hayo, siwezi kulala na sikubali kushindwa hata siku moja maana inauma kweli ambavyo Mpwapwa imeharibika,’’anasema Shekimweri.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmasahauri ya wilayani Mpwapwa Mohamed Maje anasema kuwa kuna watu wengi walio vamia maeneo ya muhimu ikiwemo hifadhi ya misitu ya asili ijulikanayo kama milima ya safu za milima ya TAO za mashariki.
Maje anasema Milima hiyo ambayo inapatikana katika Kata za Lufu na Lufusi ni milima muhimu sana kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sahihi za asili ya Mpwapwa tangu enzi za ukoloni.
Alisema kuwa uvamizi katika maeneo hayo ni mkubwa na ambao
usingepaswa kuvumiliwa hata siku moja lakini akashangazwa kuona viongozi
walioko katika maeneo hayo husika
kuendelea kuwafumbia macho.
Maje anabainsisha madhara yatakayojitokeza kwa siku za usoni kuwa ni zaidi ya watu 300,000 kukosa chakula na kushuka kwa uchumi wa familia hizo kutokana na kukauka kwa vyanzo vya maji katika milima hiyo.
Mbali na kukosekana kwa maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
Maje anabainsisha madhara yatakayojitokeza kwa siku za usoni kuwa ni zaidi ya watu 300,000 kukosa chakula na kushuka kwa uchumi wa familia hizo kutokana na kukauka kwa vyanzo vya maji katika milima hiyo.
Mbali na kukosekana kwa maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
Pia alisema lazima waunganishe Nguvu kati ya Wilaya za
Kilosa na Iringa Vijijini katika
harakati za kupambana na uharibifu wa mazingira ambapo madhara yake yanazigusa
wilaya hizo tatu.
Maje alidai kuwa kutokana na uharibifu huo Wilaya za Mpwapwa, Kilosa,Iringa Vijijini na Chamwino zinaweza kukwama katika mpango wa serikali wa umwagiliaji.
Milima ya Tao za Mashariki Wilayani Mpwapwa ndicho chanzo kikubwa cha maji ambayo hutumika katika shughuli za za kilimo cha umwagiliaji wa zao la mpunga katika bonde la Lumuma.
Bonde hilo ni maarufu kwa wananchi wa wilaya za Mpwapwa na Kilosa ambalo linalimwa zaidi Mpunga,vitunguu na mahindi na maharagwe.
Kutokna na Uvamizi huo katika milima hiyo, kumepelekea bonde la Lumuma kupungua kwa maji na hivyo wananchi wanaoishi kwa kutegemea bonde hilo hivi sasa wanaishi maisha ya ‘chungu moto’Kutokana na hali hiyo pia alisema itaadhiri mapato ya halmashauri.
MWISHO
Comments
Post a Comment