UCHAFU WATISHIA KIPINDIPINDU MTAA WA MAJENGO.
Badhii ya wananchi wakifanya usafi katika Ndampo la kwa Nzige ambalo si rasmi Ndampo hilo limepelekea MVUA kutaka kusomba nyumba ya mwl Sambae .
WANANCHI wa mtaa wa majengo katika kata ya Mpwapwa mjini wilayani hapa wamelalamikia kitendo cha uongozi wa wilaya kuweka Dampo la taka katika maeneneo ya makazi ya watu na kutishia
kutokea kwa ugojwa wa kipindupindu katika msimu huu wa mvua za vuri.
Kedmoni Mapuga mkazi
wa mtaa huo alisema kumewako na
usumbufu mkubwa na badhii ya
wakazi wa mtaa huo wenye watoto wadogo huwalazimu kuhama nyumba kutokana kukidhiri kwa taka katika mtaa na
harufu mbaya pamoja na moshi mkali pindi wachumapo taka hizo kuawathiri
kiafya na kusababisha vikohozi kwa watu
wa mtaa huo.
Mapuga alisema
baada wakazi wa mtaa wa
majengo wamekuwa wakiadhiriwa na moshi
mkali na wenye harufu kali na kutishia wakazi wa mtaa huo kupata ugonjwa wa kihozi kama bado
halimasahauri ikiendelea kuchoma taka katika eneo la korongo ambalo liko
katikati ya makazi ya watu .
Aidha Mapuga alienda
mbali na kuulalamikia uongozi wa
halmasahauri kitengo cha usafi na mazingira kwa kusema kuwa wameshidwa
kutekeleza na kuendana na kauli ya raisi
Magufuli ya kuwataka wanachi kufanya
usafi ili kuweza
kujikinga na magonjwa yanayoweza kusabaishwa na uchafu.
Pia aliema uchafu huo
unatupwa katika eneo hilo
linatishia kuweza kutokea magonjwa ya
mlipuko katika kipindi hiki cha msimu
wa mvua za masika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
mtaa huo Bi Asha Makupa alikili
mtaa wake kuadhiliwa na kadhia hiyo kitu alicho kisema kuwa takataka nyingi
zinazochomewa katika eneo hilo zinazalishwa
na wafanya biashara wa
sokoni na kuzitupa katika korongo hilo.
Bi Makupa alisema alisema suala hilo amelifikisha katika
uongozi wa halamasahauri lakini
alijibiwa kuwa chanagamoto ni halmasahauri kuto kuwa na gari la
kusombelea taka na kwenda kuzitupa kwenye eneo la dampo lililoko nje kidogo ya
mji wa Mpwapwa.
Naye katibu wa soko kuu la Mpwapwa mjini bwana Said Sadala
alikili baadhi ya taka laini kuzitupa katika eneo hilo kitu alicho kisema kuwa ni
kutoakna na kuruhusiwa na uongozi wa
mamlaka wa mji kutokanana kukosekana kwa miundo mbinu ya kubebea taka
hizo.
Kwa upande wake ofisa usafi na mazingira ya wilaya ya Mpwapwa
bwana Teodoli Mlokozi alikili baadhi ya watu kuchomea taka katika eneo hilo
kitu alicho sema tayari wamesha weka
katazo la kutupa taka katika eneo .
Aidha Mlokozi alisema pia watuwamekuwawachomea takataka
katika maeneo ya watu kitu alicho kisema
kuwa kinatokana na uongozi wa mji huo na uongozi wa halmasahauri ya wilaya
kutokuwa na magari ya kusombea taka na
kwenda kuzitupa dampo.
Comments
Post a Comment