WASTAFU WALIA KUKOSA UMOJA
Katibu
wa chama cha walimu wilayani Mpwapwa
mkoani Dodoma bwana Pankras Ngamesha
ameiomba serikali ya awamu ya tano kuwachukulia hatua waajili wanaozembea
kuwasilisha michango ya makato katika mifuko ya pesheni hapa nchini
Ngamesha alitoa kauli hiyo alipokuwa akiongea katika hafla ya kuwashika
mkono wa pongezi walimu 34 wa wilaya ya mpwapwa mkoa wa Dodoma walio stafu
utumishi wao mwezi march na mwezi
mei mwaka 2016.
Ngamesha
alisema kumekuwako na chanagamoto kubwa kwa wastafau kuishi maisha magumu mala
baada ya kumaliza utumishi wao serikali kutokana na kucheleweshewa mafaoa yao kutoka katika mifuko ya hifadhi ya
jamii (PSPF).
Aidha Ngamesha aliwakabidhi bati 20 kila mmoja walimu kumi waliostafu ambao walikuwa wanachama wa chama
cha walimu hapa wilayani kama kuwashika
mkono wa kwaheri na kutambua mchango wao wa kukutumikia chama hicho na
serikali kwa ujumla .
Mwl Ngamesha alisema kuwa kufuatia mabadiliko ya katiba ya chama cha
walimu nchini mabadiliko ya 2014 ndio
yaliyo zaa maazimio ya utoaji wa mkono
wa kwa heri kwa wananchama wake walio
tumikia chama hicho kwa muda usio pungua miezi 180 au miaka 15.
Akisoma
lisala ya wastafu kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu Mark Maganza alisema ili
kuondokana na changamoto hiyo kwa
walimu lazima chama hizo kufikirie kuanzisha
mfuko wa jamii ili kuweza kukabiliana na chanagamoto ya ucheleweshaji wa
pensenkwa wastafu wa fani ya ualimu hapa
nchini
Pia Maganza alisema pamoja na changamoto ya na wastafu kucheleweshewa mafao yao lakini pia kuna chanagamoto kubwa
inayaowakabili wastafu ni waajili kuto
kuwasilisha michango yao katika mifuko ya jamii na hivyo kupelekea kupunguza
pesheni ya mtumishi .
Hata
hivyo Mangaza alisema kuwa wastafu
wameshidwa kuwa na sauti ya pamoja na kutoa malalamiko yao kutokana na kutokuwa
na chombo cha kitaaluma cha
kuwasemea wastafu wa fani hiyo, hivyo kupelekea kila mmoja
kuitafuta haki yake kivyake na
kusababisha kuingia kwenye rushwa ili kuweza kupata haki yao au
kuwaishiwa mafao yake.
Pia
aliiomba serikali kuweza kutoa mafao ya walimu kwa wakati ambapo kwa sasa alisema huchukua muda wa
miezi tisa hadi mwaka mmoja mtumishi anapo stafu kupata mafao yake kitu alicho
kisema kuwa kwa kucheleweshewa mafao yao
kunaashiria mianya ya rishwa kwa wahusika
“Iweje
mimi najiliwa serikali inajua nimeajiliwa na siku yangu ya kustafu wanaijua
mala baada kustafu wanaanza kunisumbua kalete hiki mala hiki hii si
nikujitengenezea mianya ya rushwa tu na
usumbufu usio na sababu “aliongea Mangaza.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmasahauri ya wilaya
ya Mpwapwa Bwana Mohamed ilikili kudaiwa
na walimu hao lakini alisema tayari amesha
anzakulipa madeni ya walimu hao
na alisema wataendelea kufanya hivyo kutokana na uwezo wa halmasahauri
Comments
Post a Comment