MTENDAJI WA KIJIJI AMUWEKA MAHABUSU MWANAFUNZI KWA SIKU TATU RUDI.
KATIKA hali isiyo kuwa ya kawaida mtendaji wa jijiji cha Igunga kata ya Rudi wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma amemuweka maabusu kwa siku
tatu mtoto ya miaka 11 mwanafunzi wa darasa la tatu mala baada ya kupigana na mwezie shuleni.
Mzazi wa mtoto huyo bwana Gerard Simbai
alisema kuwa watoto hao
wanaosoma katika shule ya msingi Igunga
kata Rudi walipigina wakiwa shuleni siku ya tarehe 30,agosti mwaka huu lakini
mtoto huyo alikamatwa siku ya taehe
11,octeber mwakaa huu.
Bwana Sambai alisema baada ya kukamatwa na mgambo aliyejulikana
kwa kwa jina la moja la Dales na kumwambia kuwa
mtoto huyo anatakiwa na na
mtendaji wa kijiji kwa mahojiano zaidi aliye julikana kwa jina la
Makalios Mbada.
Aidha bwana Sambai alisema alipo jaribu kumfuatilia haki ya mwanae uongozi wa kijiji hicho
ilimtishia na kumtaka alipe gharama za
matibabu alizotumia mzazi wa mtoto walio
pigana na mwanae ili wamuachilie alipo kataa
kulipa ghalama hizo ndipo alipo chukua jukumu la kumchukua mtoto na
kwenda kumuweka chini ya ulinzi wa mgambo wa kike kwa siku tatu mfululizo.
Pia Sambai alisema kuwa tangu tukio hilo kutokea lakini uongozi huo ulikuja kumkamata mtoto
huyo baada ya mwezi mmoja na zaidi
kupita na ndipo kumshikilia na kumuweka chini ya ulinzi.
Bi Mwaka anaetumika
kama mgambo katika kijiji hicho japo hajapitia mafunzo ya mgambo alikili kumshikilia mtoto huyo kwa siku tatu
mfululizo mala baada ya kupigana na mwezie shuleni na kuumizana kwa maelekezo ya mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji.
“Kwa kweli mimi niliambiwa nikae na mtoto huyo hadi hapa
mtendaji atakapo kuja kumchukua nimekaa nae siku mbili nikaona kimya ilibidi
niende kuwambia lakini mwenyekiti wa kijiji aliniambia nikimuachilia nitafugwa
mimi ndipo nilipo enda kwa mtendaji wa kata aliye amuru mtoto huyo kuachiliwa
na kuwakabithi wazazi wake” aliongea Bi Mwaka .
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igunga mwalimu Egid Mwachali alikili siku ya taerehe 30 septemba mwakaa
huu watoto hao wakiwa shuleni na mmoja
alipiga mwezie kichwa na wote waliitwa
na kuonywa na walimu lakini suala hilo lilishia hapo
Aidha mwalimu Mwachali
alisema kwama baada muda kupita zaidi ya mwezi ndipo alipo ona
mtoto huyo huyo hakufika shuleni kwa muda wa siku tatu na alipo fuatilia
aliambiwa anashiliwana na mtendaji wa
kijiji kwa kile alicho kisema kuwa ni
kutokana na ugomvi ilio tokana na
kupigana na mwezie shuleni.
Aidha Mwalimu
Mwachali alisema kuwa” kwa mujibu
wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009
inakazata kumuweka chuni ya ulinzi mtoto yeyote chini ya miaka 18 na kumachisha masomo bila taarifa kwa kosa olote lile kitendo cha
namana hiyo ni ukatili kwa watoto lakini pia ni kuwaathili watoto
kisaikolojia”aliongea mwalimu mwachali
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Rudi bwana Harod Mkombola alikili mtoto huyo kushilikiliwa na uongozi wa kijiji cha Igunga kwa siku mbili na alisema kuwa yeye hakuwa na
taarifa baada ya kupata taarifa iliamuru
mtoto huyo kuachiliwa na kukabidhi kwa
wazazi wake.
Alisema uongozi wa kijiji hicho uliamua kumshilia mtoto huyo
baada ya kuona mtoto mwezie kulalamika kuumizwa kichwani na kuhitaji vipimo
zaidi katika hospitali ya rufaa Dodoma.
Comments
Post a Comment