WALIMU WAASWA MAADILI
Na Stephen Noel – Mpwapwa.
WALIMU watakao husikana
kusimamia mitihani ya kidato cha nne mwaka 2016 wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wametakiwa
kufanya kazi hiyo kwa kuzingatia
maadili na maelekezo wa kati
wote yanayo tolewa ili
kufanikisha kazi hiyo kufanyikabila ya kuwapo kwa kasoro zozote.
Akifungua Semina
ya wasimamizi wa mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2016 iliyo fanyika katika ukumbi wa shule ya
sekondari Mpwapwa mkuu wa wilaya ya Mpwapwa
Jabil Shekimweri amesema Serikali
ina imani kubwa na walimu hao kufanikisha zoezi hilo la kitaifa pia na wao hawana budu kuonyesha imani
hiyo kwa kutekeleza majikumu
yatakayopewa na viongozi wao pamoja na
kamati ya mtihani ya mkoa na wilaya.
Amesema dhumuni la semina
hiyo ni kuwakumbusha na kuwalekeza
wazimamizi wote wa mitihani pamoja na
wakuu wa shule kuto kufanya udanganyifu wowote wawapo katika vituo vyao vya
mitihani ili kulisaidia taifa kuweza kupata
wanafunzi halali na sahihi ambao watakao kuwa wataalamu wa baadae katika
serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Amewataka wakuu wa shule wote kwa kusaidiana na
waratibu elimu kata kuweza kuwachukulia hatua wazazi na walezi wote ambao
tayari wamewaowesha wanafunzi na
kusabisha wanafunzi hao kuacha shule.
Kwa upande wake Ofisa
elimu sekondari wilayani hapa Bi Suma
Mwapulo alisema kuwa wa mwaka
2016 jumla ya watahiniwa 1663 wanategemea kufanya mtihani wa kuhitimu
kidato cha nne ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa kujitemea .
Bi Mwapulo amesema
wanafunzi 61 wanatarajiwa kufanya
mtihani wa maarifa katika kituo cha kufanyia mitihani katika chuo cha ualimu
mpwapwa na wanafunzi 84 ni
wanafunzi kidato cha nne ambao watafanya
mtihani kama wanafunzi wa kujitemea wakatika wanafunzi 1579 ni watahiniwa wa
shule za sekonadri za serikali na za
Umma .
Comments
Post a Comment