SERIKALI ISHUGHULIKIE VYANZO VYA MADAWA YA KULEVYA SIO MATOKEO.
Na Stephen noel- mpwapwa.
SERIKALI imeswa kuachakuwekezanguvu kubwa katika kushughulikia
matokea ya madawa ya kulevya nchini bali ijikite na kuongeza nguvu katika kushughulikia vyanzo
vya madawa ya kulevya ili kuweza kuliokoa Taifa.
Wito huo umetolewa na bwana Elieza Mdakilwa mwenyekiti wa
shirika la (TUSPO)Tanzania usersand survivors psychiatry ambalo ni
shirika lisilokuwa la kiserikali la
kuwahudumia watu wenye matatizo ya akili
na kupambana na madawa ya kulevya
kwenye semina ya siku mojailiyo fanyika katika hotel Akh juu ya kuwasaidia watu wenye magojwa ya
akili.
Mdakilwa amesema kuwa
pamoja na serikali kuonyesha jitihada kubwa katika kupambana na wimbi la
madwa ya kulevya nchini bali amesema kuwa jitihada hizo zinaonyesha kujikita
kupambana na matokeo yake badala kushughulikia
vyanzo vikubwa vya tatizo hilo.
Mmoja wa wa wajumbe katika semina hiyo Bi Teresia Mnemele amesema kuwa kumekuwako na
wimbi kubwa watu wenye ugonjwa wa akili kwa sasa ambao matatizo hayo yamezi kukua siku hadi kutokana
na ongezeko kubwa la vijana kujiingiza
katika matumizi ya madawa ya kulevya
ikiwamo madawa ya viwandani na
madawa ya masahamabani .
Pia alisema “kwa sasa jamani
vijana wa kike kwa wa kiume wameharibiwa na madawa ya kulevya na kwakweli madwahaya yanathiri sana nguvu
kazi ya taiafa kwa asilimia nyingi
lakini sisi kama wananchi vyombo hivy vya kushughulikia sula hili wako wapi
mbona tunasikia wamekamata kete kumi,wale wanaokamatwa na kilo 100,mbona
hatuwaoni wakipelekwa mahakamani”alihoji
bi Teresia.
Kwa upande wake Mratibu
wa wa shirika hilo tawi la Mpwapwa bwana
Amos Nyongole alisema kuwa kwa mujibu wa mkataba wa haki za
watu wenye ulemavu inawataka nchi
wanachama ikiwamo Tanzania inawataka
nchi wanachama kuweza kufuata na kuzinagatia
mkataba huo ili watu waliokuwa kwenye kundi hilo kuweza kupata haki zao.
Aidha Nyongole alisema
mradi huo ulifadhiliwa na shirika la
Foundation for civil society imekusudia
kuamsha uelewa wa sheria ya mpya
ya afya ya akili no 21 iliyopitishwa
na na bunge mwaka 2008 ikiwa na lengo la kuhakikisha wagonjwa wa akili nchini
wanaboreshewa haki na mahitaji
yao .
Hata hivyo ofisa ustawi
wa jamii wa wilaya ya Mpwapwa Bwana
Anton Mbambile alisema kuwa lazima jamii iunganishe nguvu kupambana na
madawa ya kelevya lakini pia kuto kuwaficha na kuwanyanyapaa watu wenye
matatizo ya afya ya akili.
Pia Mbabile amesema lazima
jamii kuweza kuunganisha nguvu kuwafichua wauzaji wa madawa ya kulevya na
wazalishaji ili kuweza kupunguza
tatitizo hilo ambalo linatishia uendelevu wa rasilimali watu kwa siku za
mbeleni.
Comments
Post a Comment