WANANCHI WA IGOVU WAMTUMBUA MWENYEKITI WAO.
WANANCHI wa kijiji Igovu wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wamemtaka
mwenyekiti wa mtaa bwana Yunis Mwagowa achie ngazi kwa kujiuzuru kupisha uchunguzi kutokana na kutuhumiwa
kutumia fedha za mapato ya kijiji shilingi million moja laki tano na elfu
hamsini (1,550,000)na kutoitisha mikutano ya kisheria ya kusoma mapato na matumizi.
Mbali ya kumtaka
mwenyekiti huyo aachie ngazi pia wamemtaka
aurudishe pesa zote kiasi cha shilingi million 1550,000/= zilizotegwa kwa ajili ya kuboresha huduma za kimaendeleo
katika mtaa huo.
Hatua hiyo walifikia kwenye
mkutano wa hadahara mala baada ya mwenye kiti huo kusoma tarifa mapato na
matumizi ya mtaa huo ambapo taarifa yake
ilizua maswali mengi yaliyo kosa majibu na
kupelekea wananchi hao kuikataa taarifa hiyo na kuwataka wakaguzi wa ndani wa halmasahauri kufanya
ukaguzi maluum wa mapato na matumizi ya mtaa huo.
Akongea mmoja wa wananchi
wa kijiji hicho Paskal Mbeho aMEsema mwenyekiti wa mtaa huo amekuwa haitishi vikao
vya kisheria vya kila baada ya miezi
mitatu lakini vilikuwa havifanyiki na
kusababisha mwenyekiti wa mtaa huo kufanya maamuzi peke yake bila kushirikisha
uongozi wa mtaa.
Pia amesema katika taarifa yake inaonyesha
amenunua vitu vya kusaidia kijiji ambayo havilingani na fedha iliyotumika
na vitu vinavyo onekana katika uharisia.
Wananchi wa kiji hicho
wameenda mbali zaidi na kiutaka tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
TAKUKURU wilayani hapa kuweza
kuichunguza zaidi manunuzi hayo yaliyo
fanywa na mwenyekiti huyo kwa kile walicho kisema amenunua risiti za malipo ili
kuoanisha fedha iliyo andikwa kwenye risiti na vitu halisi.
Aidha Mbeho amesema wapo viongozi kwa kutumia madaraka waliyopewa na wananchi wamekuwa
wakijinufaisha na baadhi mapato ya mtaa huo huku wananchi walegwa wakishidwa
kupata huduma muhimu,
“Hayo ni matumizi
mabaya ya madaraka kwa viongozi ambao wamepewa madaraka na wananchi lakini wamegeuka kuwa mamwinyi na kuanza kuhujumu wananchi hivyo tunaiomba
TAKUKURU ijaribu kulichunguza suala hili”Mbeho
Kwa upande wake mtendaji wa kijiji hicho Bi Nola Rorbart amekili kuwepo kwa changamoto
hiyo kutoka kwa wanakijiji ambayo wanamtaka mwenyekiti wao aitishe
mkutano wa hadhara wa kusoma mapato na matumizi ya mtaa huo lakini bila
mafanikio.
“Ukweli ni kwamba wenye viti wa mitaa yote mitatu igovu
,Ng,ambo,na National Housing bila kutisha ilibidi mimi niitishe mikutano ya
mitaa yote ya mitaa mitatu ya kusoma mapato na matumizi lakini wananchi
wameikataa taarifa ya Igovu na sio mitaa minginezilikubaliwa”aliongea bi Norah
Pia amekili
wananchi hao kumsimamisha kwa
muda mwenyekiti wa mtaa wa Igovu wa kwa
kupisha uchunguzi hadi hapo taarifa
itakapo tolewa na alisema tayari
mwenyekiti huyo amesharudisha mihuri ofisini kwa mtendaji wa kata.
Pia lisema
kuwa suuala hilo limefika kwa uongozi wa juu wa halmasahauri na lakini
wanasubiri maamuzi ya wananchi hao.
Ukweli wenyeviti wote watatu wameandikiwa barua na
mtendaji wa kata ya kuwataka wapeleke
mapato na matumizi yote ya kijiji kwa
muda wa mwaka mmoja na kuitisha mikutano
ya hadahara ya kuwasomea wananchi mapato na matumizi mala muda
unapofika.
Hata hivyo mwenyekiti
wa mtaa huo bwana Yunis Mwagowa lakini amekanusha kutumia pesa hiyo ya
kijiji kwa maslahi yake binafsi bali alisema ni wananchi kuto kuhudhuria katika mikutano ya hadhara ambayo inakuwa inasoma mapato na matumizi.
Pia aliongeza kuwa suula hilo linapewa nguvu na baadhi wa
wapinzani wake ili kumtaka aondoke madarakani kwa hila kitu alichokisema
kuwa ni siasa chafu ambazo zinaendeshwa
juu yake.
Mwisho.
Comments
Post a Comment