WAKAZI WA MAJENGO MPWAPWA WATHILIWA NA MOSHO WA TAKA
WANANCHI wa mtaa wa majengo katika kata ya Mpwapwa mjini wilayani hapa wamelalamikia kitendo cha uongozi wa wilaya kuweka dampo la kuteketezea
taka katika maeneneo ya makazi ya watu.
Kedmoni Mapuga mkazi
wa mtaa huo alisema kumewako na
usumbufu mkubwa na badhii ya
wakazi wa mtaa huo wenye watoto wadogo huwalazimu kuhama nyumba kutokan na moshi huo kuathiri kiafya na kusababisha vikozi kwa watu wazima na
watoto.
Mapuga alisema
baada kuwa wakazi wa mtaa wa majengo wamekuwa wakiadhiriwa na moshi mkali na wenye
harufu kali na kutishia wakazi wa mtaa
huo kupata ugonjwa wa kifua kikuu kama
bado halimasahauri ikiendelea kuchoma taka katika eneo la korongo ambalo liko
katikati ya makazi ya watu .
Aidha Mapuga ameenda
mbali na kuulalamikia uongozi wa
halmasahauri kitengo cha usafi na mazingira kwa kusema kuwa wameshidwa
kutekeleza na kuendana na kauli ya raisi
Magufuli ya kuwataka wanachi kufanya
usafi ili kuweza kuweza kujikinga na magonjwa yanayoweza kusabaishwa
na uchafu.
Pia aliema uchafu huo
unatupwa katika eneo hilo
linatishia kuweza kutokea magonjwa ya
mlipuko katika kipindi hiki cha kuelekea
msimu wa mvua za masika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
mtaa huo Bi Asha Makupa amekili
mtaa wake kuadhiliwa na kadhia hiyo kitu alicho kisema kuwa takataka nyingi
zinazochomewa katika eneo hilo zinazalishwa
na wafanya biashara wa
sokoni na kuzitupa katika korongo hilo.
Bi Makupa amesema alisema suala hilo amelifikisha katika
uongozi wa halamasahauri lakini alijibiwa
kuwa chanagamoto ni halmasahauri kuto kuwa na gari la kusombelea taka na kwenda
kuzitupa kwenye eneo la dampo lililoko nje kidogo ya mji wa Mpwapwa.
Naye katibu wa soko kuu la Mpwapwa mjini bwana Said Sadala
alikili baadhi ya taka laini kuzitupa katika eneo hilo kitu alicho kisema kuwa ni
kutoakna na kuruhusiwa na uongozi wa
mamlaka wa mji kutokanana kukosekana kwa miundo mbinu ya kubebea bithaa
hiyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
mji mdogo wa Mpwapwa bwana Hamis
Hoper amekili kuchomea takataka katika
maeneo ya watu kitu alicho kisema kuwa kinatokana na uongozi wa mji huo
na uongozi wa halmasahauri ya wilaya kutokuwa na magari ya kusombea taka na kwenda kuzitupa dampo.
Comments
Post a Comment