KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDIO WAROBAIN WA USALA WA CHAKULA TANZANIA
Na stephen noel Mpwapwa .
SERIKALI ya awamu ya tano imeaswa kuwekeza katika tafiti
za kilimo na mifugo hapa nchini
ili kuweza kuwa na uhakika na usalama wa chakula kwa wanachi wake.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa utafiti
Tanzania Dr,Daniel Komuhangilo
alipokuwa akifungua warsha ya siku tatu
ya kwa watafiti
juu ya maabara za
kielektroniki iliyo fanyika katika
ukumbi wa mikutano katika chuo cha utafoti cha
TALIRI Mpwapwa.
Dtk.Komuhangilo alisema
kwa mujibu wa tafiti zilifanywa hapa nchini zinaonyesha kuwa mabadiliko ya tabia
ya nchi ni miongoni mwa sababu kubwa zinazopelekea Tanzania kushidwa kuwa na
uhakika wa chakula .
Aidha Dkt. Komuhangilo alisema
kuwa Tanzania ni miongoni wa nchi ambyo
idadi kubwa ya wanachi wake wamejikita katika sekta ya kilimo na
mifugo ambayo inakadiliwa zaidi ya asilimia 80% ya watanzania
wanajishughulisha na sekta ya kilimo na
mifugo japo kuwa bado sekta hii
haijaonyesha mafanikio makubwa sana kwa wanachi wake.
Mwezeshaji kwenye warsha
Prf. Frankwell Dule kutoka
chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine
alisema ili kuweza kuwa na kilimo
chenye tija lazima serikali iwekeze
kwenye kilimo cha umwagiliaji ambacho
pekee ndicho kitakuwa suruhisho la kuwa na usalama na uhakika wa chakula katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia
ya nchi.
Prf. Dule alisema kuwa changamoto ya uwajibikaji wa
maafisa ughani ngazi ya jamii
inapelekea sekta ya kilimo kuonekana
kuto kuonyesha tija katika miaka
yote ya uhuru wa nchi japo kuwa na kauli
mbiu lukkuki za kuhamisisha sekta ya kilimo
bila kuwapo na mikakati ya kuboresha sekta hiyo.
Hata hivyo hivyo Prf.Dule alisema chanaga moto ya mbegu feki, viwatilifu feki, na wakulima kushidwa kubadilika na kuendelea kulima kimazoea na kufuga kimazoea pia ni sababu zinazo
pelekea kilimo kushidwa kusonga mbele kwa miaka
zaidi ya hamasini sasa.
Kwa upande wake mratibu wa warsha
hiyo na ofisa maabara za
kielektonik katika tasisi ya TALIRI Mpwapwa Bi Neema Urasa alisema kuwa warsha hiyo imelenga kuwajengea
uwezo watafiti kubadilishana uzoezu kwa
njia za kielektrik kwa kusambaza taariza
za kitafiti katika machapisho ya tafiti
za kisayansi
Pia alisema njia hiyo inawasaidia
watafiti kutumia rasilimali chache ikiwemo muda, fedha, na watu ili kuweza kufikia malengo kusudiwa.
Hivyo alisema nchi zote zilizo
wekeza katika tafiti na kuzitumia tafiti
za wataalmu katika maamuzi zimesonga mbele
kimaendeleo ya jamii, Siasa
Pamoja na kiuchumi.
s
Comments
Post a Comment