VIJANA WALIO FANYA UKARABATI CHUO CHA UALIMU KUPEWA VYETI NA VETA



     
Na Stephen Noel – mpwapwa.
Naibu waziri wa elimu ya  sayansi , teknolojia  na
ufundi  Mwandisi Stella Manyanya (MB)amemtaka mkurugenzi wa VETA kanda ya kati kuweza kuwapa vyeti   mafundi  wote ambao hawajapitia veta walio weza kufanya ukarabati katika chuo cha ualimu Mpwapwa
Pia amesema ameridhishwa na ukarabati wa chuo cha ualimu  hicho,kabla hakijanza  kupokea  wanafunzi wa chuo  kikuu cha Dodoma.

     Mwandisi Manyanya aliyasema hayo  jana alipotembelea  chuo hicho  na kujionea  hali halisi ya ukarabati  kabla ya chuo hicho hakijaanza kupokea wanafunzi  wa mpango maalum  wa masomo ya sayansi walio kuwa  wakisoma  chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)  kuhamishiwa katika   vyuo mbalimbali vya  ualimu ikiwemo chuo cha ualimu Mpwapwa kwa lengo  la serikali  kukabiliana  na chanagamoto ya ualimu wa sayansi  hapa nchini.

    Pia,mwandisi Manyanya  alisema pamoja  chuo hicho kuwa cha muda mrefu  lakini serikali imeamua kuvifanyia ukarabati vyuo kumi  vya ualimu hapa nchini ambavyo vimo katika orodha ya vyuo vikongwe katika sekta ya elimu ambayo vimeteuliwa kupkea walimu wa mpango maluum wa masomo ya Sayansi.
    Aidha naibu waziri alisema baada chuo hicho kimeteuliwa kupokea walimu wa masomo ya sayansi ambapo chuo  cha Mpwapwa kinakadiliwa kupokea wanafunzi 1150 wa masomo ya Sayansi  ambao walikuwa wanafunzi wa chuo
kikuu cha Dodoma.
“Kwa kweli nimejionea kazi zinavyo kwenda na nimelidhishwa na kazi inayo fanywa hapa na chuo kimepangiwa jumla ya shilingi billion moja na million mia sita ili kukirudisha katika hali yake ya kawaida”alisema Manyanya.
Alisema katika awamu ya kwanza wizara imepanga kuwafundisha walimu 6000 ambao wataweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa walimu  wa masomo ya sayansi katika shule  za sekodari .

   Kwa upande , Mbunge wa wa jimbo la Mpwapwa George Lubeleje  alisema kuwa  chuo hicho  ni  miongoni   mwa  vyuo  vikongwe  hapa nchini  ambacho kilijegwa  mwaka 1925 na kuanza kutumika mwaka 1926 kikiwa na lengo la  kuwaandaa waafrika  kukuza elimu ya kilimo  hapa nchini.

  Hata hivyo, mkuu wa chuo cha ualimu Mpwapwa bwana Degratias Lugalema alisema kuwa  kutokana  na chuo hicho  kuwa  cha Zamani  hivyo kilikuwa kinakabiliwa
na uchakavu  mkubwa  uliokuwa unatishia  afya  za wanafunzi na wafayakazi wake.

Pia, mwalimu Lugalema alitanabaisha kuwa ukarabati uliofanywa  kwa sasa  una uwezo wa kuwapokea  wanachuo  hao kabla ya novemba 15 mwaka huu na kutoa huduma  bora ya masomo ya sayansi.
Mwandisi msimamizi wa ukarabati wa chuo hicho bwana Herbert Kimboi amesema ukarabati uliofanywa umefanywa kwa kuwatumia mafundi wazawa ambao wameonyesha kufanya kazi nzuri na gharama nafuu tofauti na wizara ingetumia makampuni ya kimataifa  na  ukarabati huo unakadiliwa kughalimu jumla ya shilingi billion 1 .6


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.