WANANCHI WA WIYENZELE WAPATA HUDUMA ZA MAJI .
Zaidi ya wakazi 3,164 wa kijiji cha Wiyenzele kata ya Chipogolo
wilaya ya mpwapwa mkoni Dodoma wataondokana adha ya kutafuta
maji umbali mrefu uliokuwa unaikabili kata hiyo kwa muda mrefu baada
ya mradi wa maji ulio kuwa unajegwa katika kijiji hicho kukamilika
na kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi kijiji hicho.
Mwandisi wa maji wilayni hapa Bi Christina Mjengi alisema kuwa kabla
ya mradi huo hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ilikuwa
mbaya ambapo wananchi ilikuwa inawalazima kutumia maji ambayo sisafi
na salama na wengine ilikuwa inawalazimu kutembea umbali mrefu
kutafuta huduma za maji.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi utaongeza ukuaji wa uchumi wa kijiji
hicho kwa watu wa matumizi ya nyumbani pamoja na unyweshaji wa mifugo
.
Aidha alisema Mradi huo umetekelezwa kwa ufadhili wa program za maji
uliogharimu jumla ya shilling milioni 341,866,135/= (million mia tatu,
arobaini na moja laki nane sitini na sita elfu na mia moja therathini
na tano.
Mwandisi mjengi alisema mradi huo utawanifaisha wakazi wa kata hiyo
wapatao 3164 sawa na asilimia 93% ya wakazi wote wa kijiji hicho na
unauwezo wa kuzalisha lita 90.000 kwa siku.
Aidha Mwandisi Mjengi alisema hadi sasa wilaya ya Mpwapwa imeweza
kufikia asilimia 51% za utoaji maji,ambapo alisema vijijini ni
asilimia 32% mijini ni asilimia 70%.
Aliwataka wananchi wa sehemu zenye miradi ya maji kuweza kutunza
mazingira na vyanzo vya maji ili kuto kuhatarisha miradi kukauka
kutokana na kukauka vyanzo vya maji unaotokana na uharibifu wa
mazingira.
Aidha alisema kuwa wameunda vyombo huru vya watumiaji maji COWSO, na
kusema kuwa kamti hizo zimeanza kazi ili kuweza kupunguza migogoro
kati ya vyombo vya watumiaji na kamati za maji.
Ameongeza kuwa katika mradi huo kulikuwa na shughuli kadhaa za kufanya
ambazo zilikuwa ni kujenga tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo lita
90,000.ujenzi wa nyumba ya kuhifadhia mashine na kujenga vituo vya
kuchotea maji, na kusambaza mtandao wa mabomba amabazo alisema zote
zimekamilika.
Mmoja wa mwanakijiji Bi Anna Chisaluni alisema kabla ya mradi huo
kukamilika wakazi wa kijiji hicho walikuwa wanatembea umabli wa km
tatu hadi tano kwenda kuchota maji katika mabwawa ya kienyeji ambayo
maji hayo hayakuwa safi na salama kwa maisha ya watu.
“ Visima hivyo ni vya kienyeji Ng’ombe ngedele mafisi ya polini
walikuwa wanakunywa hapo na kujisadia humo ndio maji waliokuwa
wanayatumia watu wa kijijini kwetu na kupelekea kuwepo kwa magonjwa
mengi ya milipuko kama kichocho na magonjwa ya tumbo”.aliongeza Bi
Chisaluni.
Pia alidai kijiji hicho kilikuwa kinakabiliwa na magojwa ya kuhara
ya mala kwa mala kitu walichokihisi kuwa kinasabishwa wakazi wa kijiji
hicho kutumia maji amabayo si salama kwa matumizi ya binadamu.
Comments
Post a Comment