CHUO CHA MAZINGIRA CHAKABILIWA NA UCHAKAVU W MAJENGO.
CHUO cha Sayansi ya Afya ya Mazingira kilichopo wilayani Mpwapwa
mkoani Dodoma kinakadiliwa na uchakavu mkubwa wa miundo mbinu ya chuo
hicho na kutishia afya wanachuo chuoni hapo.
Akitoa taarifa mbele ya mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir
Shekimweri mkuu wa chuo hicho bwana Rogasian Tarimo alisema chuo
hicho ambacho ni tawi la chuo kikuu cha Muhimbili(MUHAS) kinachotoa
elimu ya AStashahada ya Aya ya mazingira.
Bwana Tarimo alisema chuo hicho chenye wanachuo 54 kinakabiliwa na
uchakavu mkubwa wa miundo mbinu na kutishia afya za wanachuo chuoni
hapo .
Aidha Tarimo alisema chuo hicho tangu kifanyiwe ukarabati mdogo mwaka
2002 hakijafanyiwa ukarabati tena na kupelekea miundo mbinu mingi
kuchakaa na kushidwa kufanya kazi kiufanisi kutokana na kuchaa sana
.
Alisema “sisi ni maafisa wa afya ya mazingira ninaowafundisha ni
wataalamu wa afya ya mazingira sasa uchakavu huu hauendani na maudhui
ya chuo kwa maana miundo mbinu ya vyoo imechaa,vyumba vya madarasa na
mabweni hivyo kuniwia ngumu sana utekelezaji wa majukumu ya kila
siku”aliongea
Hata hivyo tarimo alisema pia chuo hicho kuto kuwa na hati ya umiliki
wa ardhi kunachangamoto ya uvamivi wa maeneo ya chuo na kutishia
kutokea kwa migogoro kati ya chuo na watu na tasisi zilizo vamia
maeneo ya chuo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri
alisema pamoja na chuo hicho kukabiliwa na chanagamoto Lukuki
zikiwamo za watumishi ameutaka uongozi wa chuo hicho kuongeza nguvu
ya kukitangaza chuo hicho ili kuweza kuwa na watalaamu wengi katika
sayansi ya mazingira ambao kwa sasa taifa na dunia wanahitajika sana,
Pia Shakimweri alisema kuwa kwa kushirikiana na uongozi wa chuo hicho
watajitahidi kushughulikia baadhi ya chanagamoto zikiwemo za watumishi
kama dreva halmasahauri kuwaazima dreva wa chuo hicho ili kuweza
kuokoa gari ya chuo hicho kuendelea kuchakaa bila kutumika kwa kigezo
cha kuto kuwa na dreva wa kuliendesha gari hilo.
Comments
Post a Comment