VIJANA WACHANGAMKIA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA.
Idadi kubwa ya vijana wajitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa ndani ya Chama cha mapindinduzi (CCM) Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Katibu wa chama hichoi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma Bi.Rukia Hassan amedhitisha hilo kuwa idadi kubwa wa
watu waliochukua fomu za kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi ndani ya chama ni kubwa ni vijana
.
Bi Rukia amesema kuwa mchakato wa uchaguzi ulioanza mwezi April mwaka huu katika ngazi za mashina na kudhibitisha kuwa fofauti na miaka iliyopita ambapo wanachma wengi wamejitokeza
kugombea nafasi zauongozi ndani ya chama kwa kile alicho kisema kuwa ni
kiashiria cha Imani ya wanachama kurudi
kwa chama.
Aidha amesema pamoja na kukua kwa imani ndani ya chama pia ni
kuongezeka kwa uelewa Demokrasia ndani
ya chama pia kupunguza vikwazo vilivyo kuwa
vinakuwa kipingamizi kikubwa cha wanachamakuingia katika nyadhifa
mbalimbali ikiwemo Rushwa,Kujuana na Upendeleo.
Pia Bi Rukia amesema kuwa Imani ilionyeshwa na mwenyekiti wa chama
Taifa ambaeni Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuri imeweza kurudisha Imani ya
vijana kurudi ndani ya chama na kugombea
nafasi ndani ya chama.
Hata hivyo Bi Rukia amewahadaharisha wagombea wote watakao kiuka taratibu na kanuni cha uchaguzi kuondolewa
katika kinyang’anyilo hicho.
Pamoja na idadi kubwa ya wanachama hao kujitokeza kuchukua
fomu kwa wingi chombo hiki kimebaini kuwapo kwa
changamoto ya kubaguana kijimbo kitu kinacho ashirilia
kumeguka kwa chama.
Comments
Post a Comment