WANANCHI WA MLEMBULE WATEMBEA UMBALI WA KILOMETA 40 KUTAFUTA HUDUMA ZA AFYA.
www.facebook.com
WANANCHI wa kijiji cha
kijiji cha Mlembule wilaya ya Mpwapwa
Mkoa wa Dodoma Huwalazimu kutembea umbali wa kilometa 12 hadi 40 kufika
makao makuu wa wilaya kutafuta huduma za afya kutokana na kijiji hicho kuto kuwa na kituo cha afya katika kata hiyo kinachoweza kutoa huduma ya
uapasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Andason Mwangalimi alisema
hali hiyo imekuwa ikiwaathili
sana akina mama wajawazito wanapougua
usiku au ugonjwa wa ghafla.
“Kutokana na hali
hii akina mama huwalazimu kutembea
umbali wa kilomita 12 hadi 40 kwasabu
kijiji hiki hakina zahati na kipindi cha mvua kijiji hiki kinakorongo
kubwa lijulikalo kama korongo la manamba
maji yakijaa watu hushidwa kuvuka na kuna mama mjamzito aliwahi kufia
hapa kutokana na kukosa huduma kwa muda muafak”aliongea .
Bwana Mwangalimi alisema kutokana na hali
hiyo akina Mama wajawazito wamekuwa wakijifungulia njiani na porini
kutokana na kuwepo wa vituo vya
afya.
Mmoja wa wananchi wa kata Bi Eva Deo alisema katika kipindi cha masika wananchi wa kijiji hicho
wanalazimika kutumia dawa za mizizi ili
kuweza kuokoa maisha yao kipindi cha masika .
Pia alisema kutokana kata hiyo huwalazimu watoto kuwapima
uzito kwa kufunga mzani kwenye miti.
Mhuduma wa afya katika
kata hiyo Bi Halima Maganga alikiri kutoa huduma ya fya kwenye mti wa
mkwaju aliopo kwenye karibu ofisi ya kijiji na alisema kwa mwezi mmoja
anapima watoto 1400 hadi 1600.
Pia alisema akina mama wajawazito kukosa faragha ya kupimwa kutokana na
kupimwa kwenye chumba kidogo kisicho kuwa usiri na hadi ya kuwapimia akina mama
wajawazito.
Bi Maganga alisema hata kama kuna mjamzito anahitaji msaada
wa haraka hushidwa kupatiwa msaada huo
na kusababisha akina mama wengi wa kijiji hicho
kujifungulia kwa wakunga wa jadi na
majumbani kutokana na umbali wa huduma za afya zinako patikana.
Pia alisema akina mama wengi wamekuwa wakipata ugonjwa wa
fistula kutokana na wengi kukaa na uchungu mda mrefu pindi wanapo
safari,kukosa huduma za afya , na sehemu rafiki za kujifungulia.
Diwani wa kata hiyo
bwana Willison Mgunga alisema kata
hiyo tayari imesha
jenga msingi wa jengo la zahanati
na wameshafyatua matofali 2748 ya
sementi tayari kuanza kupandisha ukuta wa zahati ya kijiji hicho.
Hata hivyo Mgunga
alisema katika baeti ya halmasahauri ya mwaka 2017/2018 wametinga kiasi cha
shilingi million 42 kwa ajili ya kuborsha huduma za afya katika kata yake.
Comments
Post a Comment