DC MPWAPWA AOBWA KUINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI NDUGA.
WANANCHI wa kijiji cha Nduga kata
Mlembule wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma wameiomba kamati ya ulinzi na usalama
kuingilia kati mgogoro wa mashamba katika bonde la kijiji hicho unatishia uvunjifu wa amani.
Akiongea mmoja wa wananchi wa kijiji
hicho na mwenyekiti CCM wa kijiji hicho Tumain Yohana amesema kumewako hali ya sinto fahamu kutoka mtu mmoja aliya fahamika kwa jina la Rashid
Sudi Makasi kwa wanachi
kile alicho kisema kuwa kunatishia wananchi hao kuwafukuza kwa kuwafukuza katika
maeneo yao kwa kudai kuwa ni yake.
Bwana Tumaini amesema alisema kuwa kijiji cha nduga kimeanza
kulitumia shamba hilo zaidi ya mika arobaini
iliyo pita na ilikuwa moja wapo ya chanzo cha mapato ya kijiji hicho
ambapo wanannchi walikuwa wanakodishwa na kulipa kiasi kidogo kwa kijiji na
sasa shmba hilo linataka kunyanganywa na bwana sudi kwa lengo la yeye kutaka kuwakodisha wanakijiji hao.
Mwanakijiji mwingine aliyejitambulisha kwa
jina la Hashimu Idd Risasi aMEdai kuwa
kijiji hicho kimaenza kumiliki eneo hilo kabla ya Tanganyika haijapata
uhuru mwaka 1959 lakini mwaka 2014 alijitokeza
mjanja mmoja ambae anawanunua viongozi wa kijiji na kutaka kupora eneo la
serikali ya kijiji ambayo ni shamba la ujamaa tangia nchi hii inaitwa
Tanganyika”aliongea
Bwana Risasi amesema kuwa kwa sasa wameiomba serikali ichukuehatua za
haraka kabla ya hali haijawa mbaya.
.Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo bwana Willson Mgunga amekili
kuwepo kwa mgogoro ambao alisema kwa sasa unatishia amani ya kijiji hicho
na bwana Sudi.
Bwana Mgunga ameiomba serikali kuchunguza nyaraka alizo kuwa nazo bwana Sudi
juu ya umilikiwa eneo hilo kwa kile
kinachoaminiwa kuwa ni hati feki. Na kulipatia ufumbuzi wa haraka ili lisije
kuleta madhara.
Alipo ulizwa juu ya tuhuma zinamkabiri
bwana Rashid Sudi Makasi amekanusha
kuwanyanganya wananchi mashamba yao bali alisema maeneo hayo ni yake ya urithi
wa baba yake na alisema “kwa yeyote anae dai kuwa eneo hilo ni lake aende
mahakamani ndiko watakakoenda kutoa haki”.aliongea Bwana Sudi.
…………………………………
MWISHOOOOOOO………………………
Comments
Post a Comment