WAIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI WAASWA KUFUATA MAADILI.
.
WAIMBAJI wa nyimbo za dini Nchini wamekumbushwa kutunga
nyimbo za kuhamasisha Amani na watu
kupenda kufanya kazi.
Sambamba na hilo pia waimbaji wa kike wa
Music wa dini wametakiwa wasimame katika uwakili wa kazi ya Mungu
ya kuomba kwa ajili ya Taifa na
kuombea familia na kubaki katika maadili ya music wao unavyo wataka .
Rai hiyo imetolewa jana wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma na Meneja wa Bank ya NMB
tawi la Mpwapwa Bi Beatrice Mwasa
katika Uzinduzi wa Album ya
mwimbaji wa nyimbo za Dini
Mwalimu Paulina Ndatila(Mwl Boma)
albam inayojulikana kwa jina la TUTATAWALA.
Bi Mwasa alisema kumekuwako
na upotovu wa maadili kwa baadhi
ya waimbaji wa nyimbo za dini kwa uvaaji wao ambao hauakisi kile wanacho kiimba
Pia alisema waimbaji hao wakitunga nyimbo za njisi ya
kupunguza migogoro ya familia ambayo inatishia kuongezeka
kwa uvunjifu wa amani kuanzia ngazi ya familia hadi taifa .
Aidha Bi Mwassa alisema kama akina mama wakisimama katika
kazi uwakili wao wa kuzilea familia
,kukaa na watoto wao, na kuongea nao
kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza vitendo vinavyo tokea katika faifa
kwa sasa katika familia na ndani ya
makanisa .
Bi Mwasa alisema
musiki wa nyimbo za Dini kwa sasa
ni miongoni mwa music unasikiizwa na
watu wengi hapa nchini hivyo waimbaji watumie fursa hiyo
kuhamasisha Amani na uwajibikaji kwa kufanya kazi “maana hata
maandiko yanasema asiyefanya kazi na
asile,pia maandiko yanasema kuweni na amani
na watu wote” aliongea .
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Benki ya Posta mkoani Dodoma bwana Halfan Twaha alisema Music
ni fani inayochukua kundi kubwa la
vijana na na watu wazima “ hivyo kuna
haja ya serikali kuiwekea mazingira rafiki fani hii ili iweze kuzalisha ajira kwa vijana wengi wenye vipaji vya
uimbaji hapa nchini” aliongea
Pia alisema kwa sasa Banki
ya posta ambayo iko kwenye malekebisho makubwa inajipanga kufanya kazi na
makundi yote wakiwamo wanamusic,wakulima ,wafanya biashara pmoja na makundi yote ya watu wanaotaka
kujiwekea akiba katika benk Posta Tanzania.
Comments
Post a Comment