SERIKALI YAWAPA MTIHANI WAKUU WA SHULE MPWAPWA
SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imewataka wakuu wote shule
zote za kidato cha sita zilizopatiwa fedha za ukarabati kuthaminisha
ukabarabati wa shule hizo sambamba na uboereshaji wa elimu katika
shule zao.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri
alipotembelea shule hizo kwa ajili ya kuangalia hali halisi ya
ukarabati unaoendelea katika shule hizo.
Shule zilipatiwa fedha za ukarabati katika shule za kidato cha sita
ni Mpwapwa Sekondari ,Mazae Sekondari,Berege sekondari na Kibakwe
Sekondari.
Shekimweri alisema hakuna zaidi kwa shule hizi kutoa shukrani kwa
serikali zaidi ya kupandisha kiwango cha ufaulu katika shule zote
ambazo zimepatiwa fedha za ukarabati.
“haiwezekani shule zinapendeza zinanga’aa lakini ufaulu unakuwa chini
hivyo wakuu wa shule na walimu mjipange sasa uzuri wa miundo mbinu
hii ya shule iendane na viwango vya elimu vinavyo tolewa shuleni hapa
tunataka kusiwe na division four wala three hapa tuanzie division
two ndo itakuwa shukrani kwenu kwa serikali” aliongea.
Shakimweri alisema serikali imetoa zaidi ya billion mbili kwa ajili ya
ukarabati wa shule zote za kidato cha sita kwa ajili ya kuboresha
miundo mbinu ya kujifunzia na kufundishia.
Kaimu mkuu wa shule ya Mpwapwa Sekondari Mwalimu Omary Towaqali
alisema Shele hiyo ambayo imejegwa mwaka 1926 ambayo haikuwahi
kufanyiwa ukarabati tangia ijegwe kwa zaidi ya miaka 90 hivyo
kupelekea uchakavu mkubwa na kutishia afya za wanafunzi shuleni hapo.
Aidha alisema kwa kukamilika kwa ukarabati na ujenzi wa bweni jipya la
wanasichana wa kidato cha tano na cha sita kutawasaidia wasichana hao
kupata malazi mala baada ya bweni la wanafunzi hao kuungua moto
January 20mwaka 2015 wanafunzi wa kidato cha sita cha tano wasichana
iliwalazimu kulala kwenye darasa lililokuwa chumba cha kopyuta
kutokana na bweni hilo kuungua moto.
Pia mkuu wa shule hiyo alisema shule inakabiliwa na uchavu mkubwa wa
miundo mbinu ya shule ikiwemo majengo, matundu ya vyoo na vyumba vya
maabara za masomo ya sayani pamoja na vifaa vya kufundishia.
Mwandisi wa wa anayesimamia ukarabati katika Shule ya sekondari
Mpwapwa bwana Herbert Kimboi aisema ukarabati huo unatarajiwa
kukamilika kabla ya july 15 mwaka huu na ukarabati huo unakadiliwa
kutumia jumla ya shilingi bilioni 1.2/=ambapo alisema mpaka ukarabati
huo umetumia jumla ya shilingi million 700 na kwa kutumia mafundi
wazawa wameweza kuokoa julma ya shilingi zaidi ya million 518,
Alisema ukarabati huo ni mpango serikali wa ukarabati kwa shule
kongwe hapa nchini kupitia wizara ya elimu katika mpango wake wa
lipa kutokana na matokeo.
Mwandisi Kimboi alisema kwa sasa ukarabati wa shule hiyo umefikia
asilimia 90% na hatua iliyobaki ni umaliziaji wa vitu vidogovidogo
kama usafi na uapngaji wa vitanda tayari wanafunzi wafuanguapo shule
july 15 wayatumie madarasa hayo na mabweni hayo.
Shule ya sekondari Mpwapwa ni miongoni shule kongwe hapa nchini iliyo
jegwa mwaka 1926 na serikali ya kikoloni ikiwa na lengo la kuwaandaa
watoto wa machifu kuja kufanya kazi katika serikali yao yao ,kwa
kipindi hicho kazi hizo zilijulikana kama white colar job
Comments
Post a Comment