WAWEZESHESHAJI WA TASAF WATAKIWA KUSIMAMIA TARATIBU
WAWEZESHAJI wa wilaya
katika mpango wa TASAF awamu ya
Tatu wametakiwa kusimamia
taratibu na kanuni za mpango
huo ili uweze kuwanufaisha walegwa kama
ilivyo kusudiwa na serikali.
Kauli hiyo ilitolewa na
afisa ufuatiliaji wa mpango huo wilayani hapa Fraston
Anyitike alikuwa akingea na wawezeshaji wa wialaya katika mpango wa malipo juu ya kuwezesha kaya maskini katika kipindi cha roya ya march
-April 2015.
Anyitike amesema japo kuwa
utaratibu unafahamika lakini wapo baadhi
ya watendaji wa vijiji wamekuwa
wakitumia fulsa hiyo kuwaingizia wanachi michango mbalimbali ambayo haipo katika mpango wa
vipaumbele vya ruzuku hiyo
kwa walegwa.
Amesema kuwa ruzuku ya wanayao pokea walegwa katika
mpango wa TASAF awamu ya
tatu imelenga kuboresha elimu na afya kwa kaya hizo na kuongeza kipato kwa kaya
maskini kupitia uwekaji wa akiba na kuwekeza katika shughuli
za kiuchumi kama ufugaji wa kuku wa kienyeji ,ufugaji wa nguruwe na mbuzi kwa
kaya hizo ili ziweze kuboresha maisha.
Mmoja wa wanufaika wa mpango katika kijiji cha iyenge Bi Maria
Vitalo amesema pamoja na Tasaf
kuhamasisha walegwa kukata bima wamejitokeza
kukata bima hizo lakini tatizo tangu
wakatiwe bima hizo hawajapewa
vitanbulisho vya matibabu na
hivyo kuendelea kununua dawa katika
maduka ya dawa wakati walikata bima miezi mitatu iliyo pita.
Mtendaji wa kijiji hicho Enock
Kinoga amesema kumekuwako na changamoto ya ya ukosefu wa vifaa vya kutengenezea vitambulisho hivyo na alikili kuwepo kwa
usumbufu mkubwa kwa wanachama hao kushidwa kupata huduma katika vituo vya afya
kutokana na kukosa vitambuliso .
Kaimu mratibu wa mfuko wa afya ya
jamii wilaya Bwana Musa Pima amekili
kuishishiwa vifaa hivyo ikiwemo
karatasi za kugundishia
zijulikanazo kama lamination kitu alicho kisema tayari wamesha pokea karatasi hizo
na wamesha anza kuzisamabaza katika
vituo mablimbali hapa wilayani.
Comments
Post a Comment