BILION MOJA ZATOLEWA KAMA MKOPO NA FINCA MPWAPWA
Na Stephen noel –Mpwapwa.
JUMLA ya shilingi
bilioni moja na na million
miatano zilitolewa kama mkopo mbalimbali na Benk Finca tawi la Mpwapwa Mkoa wa Dodoma kwa wateja
wake wapatao 2000 kwa mwaka 2013/2014.
Kauli hiyo ilibainishwa na meneja
wa Finca tawi la Mpwapwa Bw,Edson Joel alipokuwa akiongea na waaandishi wa
habari ofisini kwake jana
kwa mahojiano maluum.
Joel alisema mikopo walioyo itoa
ni kwa ajili ya biashara kwa wafanya biashara
wakubwa wa kati, na wajasilia mali wadogo wa wilaya ya mpwapwa.
Meneja huyo alisema Lengo la
Benk hiyo ni kukuza
biashara na kuimarisha uchumi kwa
jamii na pia kuondoa umaskini kwa watanzania ambao
wengi wao hufanya kazi ya
kupambana na umaskini lakini hukabaliwa na chanagamoto ya ukosefu wa mikopo
na elimu ya ujasilia mali .
Amesema wao kama wadau
huwasaidia serikali katika kutekeleza malengo ya mileniam na kuweza nchi
ya T anzania kufikia kipato cha kati
ifikapo 2025 ili kuweza kupunguza
umaskini wa kaya na jamii kwa
kuwasaidia wengi hasa akina mama
kuweza kumiliki biashara zao.
Mmoja wa wa
wajasilia mali ambae hakutaka jina lake
lifahamike alisema Tasisi nyingi za kifedha hazina lengo la kuisaidia wajasilia
mali bali wamelenga kujinufaisha zaidi
na kupata faida kubwa kutoka kwa wateja
wao wanaowahudumia
Alidai kuwa Tanzania
huenda ikashidwa kufikia malengo yake ya Milenium na Mkakati wa kuondoa na
kupunguza umaskini tanzania kutoaka na
Tassisi nyingi za kifedha kutoza riba
kubwa kwa wajasilia mali wadogo
wanaokopa katika tasisi hizo.
Alisema lengo ambalo
hupatiwa wasiwasi wa kuto kufikiwa ni lengo la kwanza la mileniamu linalo dai
kuondoa umaskini wa kipatao na njaa na
kwa kutuza riba kubwa zaidi
ambayo ni digiti mbili kitu alicho iomba
serikali kuzitembelea tasisi hizo
na kujua mifumo ya Tasisi hizo.
Aidha Joel alisema kuwa mbali
ya kuwa na akina mama wengi
wenye uhitaji mkubwa wa kukuza uchumi
wa familia na jamii lakini wanakabili na na changamoto kubwa ya mfumo
dume unaoikandamiza jamii hasa mwanamke kuruhusiwa kuingia katika
tasisi za kifedha na waume zao kutokana na uelewa mdogo wa wanaume juu ya benk ya finca
.
Alisema mikopo walio itoa kwa wakazi wa Mpwapwa
umesaidia kubadilisha maisha ya wakazi hao kwa kukuza biashara zao na
kuweza kufanya shughuli zingine za kmaendeleo kama kusomesha watoto na
kujenga nyumba bora.
Pia aliongeza
pamoja na mafanikio hayo bali
wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo watanzania wengi kuto kuzitumia tasisi za kibenki katika kutunza fedha zao
kitu alichokisema kuwa kinaongeza
uhalifu katika jamii na mauwaji kutokana
watu wengi kutunza fedha majumbani.
Alisema kuwa
kwa mujibu wa tafiti zilizo fanywa na
Benki ya kuu ya Tanzania ni
asilimia 14% tu ya watanzania ndio
hutumia tasisi za kibenk katika kutunza
fedha zao.
Amedai kuwa jamii iondoe dhana ya kuwa
Finca hutoa riba kubwa kwa mikopo yao kitu alichokanusha kuwa benk hiyo hutoa riba kidogo ambapo alisema
kila laki moja atakayo chukua mteja
hulazimika kulipa shilling 3000 kwa
mwezi ambayo alisema sawa na shilingi elfu 18,000/= kwa miezi sita.
Meneja huyo amewataka wana Mpwapwa
ambao ni jamii wa wafugaji kuweza kuvuna
kwa kupunguza mifugo yao kuweka fedha
benk ili kuweza kujipatia kamisheni za faida kwenye akaunti ya malengo.
Comments
Post a Comment