SERIKALI YATAKIWA KUSHIRIKISHA SEKTA BINAFSI KATIKA UPANGAJI WA MIPANGO.
Na Stephen Noel -Mpwapwa.
SERIKALI imeobwa
kushirikisha sekta binafsi katika upangaji wa mipango mbalimbali ya kimaendeleo
ili kuweza kuwa na nguvu moja katika
kuzikabili changamoto za kimaendeleo zinazotokana na serikali kuto shirikisha sekta hiyo.
Lai hiyo imetolewa na Bwana
Dornard Liya mshuari wa mradi wa
kuboresha mazingira ya
uwekezaji na biashara Tanzania unaotekelezwa na shirika la Denmark
katika mikoa ya Dodoma na Singida alipokuwa akiongea na wafanya
biashara wilayani mpwapwa mkoani Dodoma.
Dornard alisema kutokana na utafiti uliofanywa na
shirika hilo ulibaini kuwa katika
nchi ya Tanzania kumekuwa na
mazingira magumu ya ufanyaji wa
biashara kwa wafanya biashara unao
tokana na kulundikiwa kodi kandamizi kwa wafanya biashara hao na kutoshirikishwa katika upangaji wa mipango mbalimbali ya serikali
kwa sekta binafsi.
Aliongeza kuwa historia ya
ya nchi yetu ya ujamaa na kujitegemmea pia imeadhiri kutozipa kipaumbele
sekta binasfi katika upangaji wa mipango ya serikali kitu alicho kisema kuwa
kinapelekea kuwepo malalamiko mengi kutoka kwa sekta hiyo kwa serikali.
Pia aliongeza kuwa kuwepo
kwa baadhi ya sheria ndogo za kodi za
halmashauri zimekuwa kandamizi na
kupelekea wawekezaji wengi kuyakimbia mazingira ya kuwekeza katika
halmashauri nyingi hapa nchini kutokana na urasimu kwa baadhi ya watendaji wa
tasisi hizo
Hata hivyo alisema tafiti
zinaonyesha kuwa Tanzania imekuwa inashika
kuanzia nafasi 145 kati ya nchi 189 duniani
kitu alichokisema kuwa kinasababishwa na urasimu wa Sera, sheria na kanuni
za biashara nchini.
Hivyo aliwataka wafanya bishara wilayani hapo kuweza kuunda
baraza la biashra la wilaya ili kuweza kufanya ushawishi na utetezi
juu ya sera, na sheria kandamizi
za kikodi.
Kwa upande wake
mwenyekiti TCCIA wilayani mpwapwa mkoani
Dodoma bwan Ben Mosha alisema wafanya biashara kuto kuwa na umoja umekuwa ni kikwazo cha wafanya bishara hao
kukosa sauti ya pamoja juu ya kufanya
ushawishi na utetezi kwa sheria
zinazotishia uendelevu wa bishara unaotokana na mlundikano wa Kodi.
.
Mmoja wawafanya biashara mdogo wilyani hap Judith Tomas alidai
kuwa Kikwazo kikubwa cha wafanya biashara wilayani hapo kushidwa kukua kiuchumi ni kukosekana kwa miundo mbinu ya kuaminika
hasa barabara za kuiunganisha wilaya hiyo na barabara kuu ambayo walisema ingeweza
kuwa kichocheo kikubwa cha wawekezaji kuwekeza katika wilaya hiyo.
Alisema kitu hicho ndicho kinachoifanya wilaya hiyo kuonekana kama iko ndani ya kisiwa na kuanza kuzidiwa
kimaendeleo na wilaya amabazo zimezaliwa kutoka katika wilaya hiyo kama wilaya ya Kongwa.
Magnus Msafiri alisema
kuwa pamoja na wafanya biashra wa
wilaya hiyo kukwazwa na kuto kuwepo kwa elimu ya kikodi kwa wafanya biashara hao
pia kumekuwako na mahusiano hasi kati
wafanya biashara hao na watumishi
wa halmashauri hiyo .
Alisema japo kuwa
Mpwapwa ina fulsa za kutosha juu ya uwekezaji lakini viongozi wa wilaya hiyo kuto fungua milango
ya uwekezaji na kuitnagza wilaya hiyo
pamoja na fulsa zinazo
patikana ndani ya wilaya hiyo imekuwa ni
sababu ya wilaya hiyo kusua sua kimaendeleo.
Pamoja
na kikao hicho viongozi hao waliweza kuteuwa uongozi utakao weza kuunda
baraza la bishara la wilaya ambao ni ,Ben mosha, Efrahim George,Monica
Lumambo,Joseph Mnemele, na Efrasia Mrema.
Comments
Post a Comment