TASAF YASAIDIA KAYA MASKINI 6288 MPWAPWA
Na Stephen noel – MPWAPWA
HALMASHAURI ya wilaya ya
mpwapwa mkoani Dodoma imeanza kunufaisha kaya maskini 6288zenye kipato cha chini
kwa kuzipatia fedha za kujikimu
kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF awamu ya nne.
Gazeti hili limejaribu kutembelea
kaya maskini katika vijiji
mbalimbali vilivyo kuwa chini ya mrad na
kukutatana na walegwa ambao walikiri
mpango huo tangu uanze kutekelezwa umeweza kubadilisha maisha yao na sasa kuyaona kuwa maisha yao yamekuwa na
unafuu tofuati na hapo awali.
Mmoja wa wanakijiji cha
vighawe kata ya vighawe Mery Mazanda amesema awali
alikuwa ankula mlo mmoja kwa siku
lakini tangu mradi huo uanze
kutekelezwa nay eye kuingia kwenye mpango kumeweza kubadilisha maisha yake
na afya yake imeboreka kwa kuweza kula milo mitatu kwa siku.
Amedai ‘”kuwaa sasa anaishukuru serikali ya Tanzania
kwa maana isingekuwa hivyo sisi
wanyonge tungekuwa tumekufa maana nilikuwa nakula mlo mmoja wa siku tu na siku
zingine tangia asubu hi hadi asubuhi
nyingine bila kula kitu kipindi cha ubuyu nilikuwa nashindia ubuyu
ambao bila kula chakula unalevya, kwa kweli
sasa naishukuru mno serikali ya Kikwete”.
Mwezeshaji wilaya Protasia Makumbo amewataka wanufaika hao kuweza kuanza kubuni miradi
mbalimbali ya kufuga kuku ngombe na
nguruwe ili waweze kuwa na miradi
endelevu.
Pia diwani wa kata ya vighawe
Dikson Mahuwi amesema kuwa mpango huo umewasidia wanufaika wengi ambao sasa
wengi wao wameonyesha mabadiliko makubwa
kwa kujenga nyumba bora, kuibuia miradi midogomidogo ambayo wanaitumia ili
kuweza kujikimu katika maisha yao ya kila siku.
Mratibu wa Tasaf
wiliya ya Mpwapwa Bahati Magumula
alisema katika robo ya nne Watoa
ruzuku kwa kaya 6288 zitakazo
nufaika na mradi huo kwa kaya maskini zilizo ibuliwa kwenye zoezi la uandikishwaji wa zoezi hili hapa awali.
“Kwa awamu hii tunatoa ruzuku hii
kama shughuli za kawaida kwa robo hii
ambapo tutatoa kiasi cha shilingi million 190.3 kwa kaya legwa 6288”alielieleza
Magumula
Aidha Magumula
alisema hapa awali kuna baadhi ya kaya zilikataa kuingia kwenye zoezi
hili lakini baada ya kuona mafanikio kwa wenzao wameanza kusumbua na wao kutaka
kuingia kwenye mpango ambapo inachukua
muda mrefu sana kurudishwa kwenye
mpango.
Kwa upande afisa Ufuatiliaji wa Tasaf wilayani hapa Fraston Anyitike amesema kwa kushirikiana na watumishi wa
halmashauri kuweza kutoa elimu juu ya
matumizi ya kifedha hizo
ili zilete tija
kwa kaya hizo maskini kwa kipindi
chote cha utekelezaji wa mradi.
Comments
Post a Comment