C WT YAPATA VIONGOZI WAPYA MPWAPWA.
CHAMA chama cha walimu wilayani mpwapwa mkoani DODOMA kimepata
viongozi wake wapya watakao kiongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano toka sasa.
Viongozi hao waliopatikana
kupitia kuchaguliwa na mkutano mkuu wa
chama hicho, uliofanyika jana katika
ukumbi wa chuo cha walimu mpwapwa mjini
hapa .
Akifungua mktano huo mkuu wa wilaya ya mpwapwa Dr Jasmini Tiisekwa alisema ni vyema walimu hao wakatumia haki yao
ya kikatiba, kuwachagua viongozi
wao ambao wataweza kushirikiana katika
harakati za kumkomboa mwalimu na katika
kuweza kujiletea maendeleo endelevu.
Aidha Dr, Tiisekwa
aliwaasa viongozi wa chama cha walimu hao kuweza kusimamia haki
na wajibu wa wanachama wao ili
kuweza kupunguza hali ya kutishia kwa
kutoweka kwa amani hapa nchini kwa madai ya kudai haki kwa migomo na
maandamano.
Pai mkuu wa wilaya huyo aliwataka walimu na wagombea hao kuweza
kuendesha kampeni za kistarabu ili kuwa mfano wa kuigwa na makundi mengine
ambayo wanaotumia demokrasi ya
kuchaguliwa kwa kuto kubali vitendo vya fujo ,matusi,na kejeli wakati wa
kampeni.
Msimamizi wa uchaguzi huyo Comred
Mwl David Kisamo alisema nafasi zinazogombewa ni nafasi ya mwenyeki wa chama , mhasibu wa
chama nafasi ya mwakilisi wa shule za sekondari, mwakilishi wa vijana na
mwakilishi wa walemavu.
Nafasi nyingine alisema ni nafasi
ya uwakilishi wa walimu shule ya msingi,uwakilishi wa nafasi ya vyuo vya ualimu na nafasi za tasisi za elimu na uongozi.
Katika matokeo hayo Comred Mwl .Daniel Tito
ndiye aliyechaguliwa kuwa
mwenyekiti na kuchukua mikoba ya aliye kuwa mwenyekiti wa chama hicho Richard
Kipalamoto, nafasi ya mhasibu wa chama hcho ilichukuliwa na Mwl Kessi Kidifu
aliyeitetea nafasi yake kwa kumshinda
mpinzani wake mwl George Ntale.
Hata hivyo nafasi ya uwakilishi wa shule za awali ulichukuliwa na mwalimu Paskali Gailanga,nafasi ya uwakilishi wa
nafasi za vijana ulichaguliwa Faustine
Chiwanga, nafasi ya uwakilishi wa walimu shule ya msingi alichaguliwa mwl Samson Kempanju na Albart Timatuku nawakati uwakilishi
wa tasisi za elimu ilichukuliwa na Mwl
Pendael Lesso.
Pia nafasi ya ya uwakilishi wa
nafasi ya wanawake ilichukuliwa na Renatha Chawene , nafasi ya uwakilishi
sekondari ilichukuliwa na mwl Michael
Mbalasalo na nafsi ya na uwakilishi walemavu ilichukuliwa na Mwl Aidani Masima
Akitoa shukrani baada ya kuchaguliwa mwenyekiti huyo Mwl Daniel Tito aliwataka
walimu hao kuweza kushirikiana katika
kujiletea maendeleo chanya na kupigania haki za mwalimu ambazo zimeonekana kuupunjwa kila kukicha
.
Comments
Post a Comment