MADREVA WA BODABODA WAPIGWA MSASA MPWAPWA.
Na Stephen noel mpwapwa.
MADEREVA wote wa naoendesha
vyombo vya moto wametakiwa kuzingatia
sheria na alama za
barabarani ili kuweza kupunguza ajali
sisizo kuwa za lazima kwa lengo kuakoa maisha ya watu na mali zao.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wa usalama barabarani wilyani mpwapwa Josephat Mjema alipokuwa akifungua
mafunzo ya siku saba ya waendesha vitu vya moto na wamiliki wa vitu vya moto na
mafunzo yanayoendeshwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la APEK.
Aidha Mjema alisema
jeshi la polisi limeingia mkataba
na shirika lisilokuwa la kiserikali
la APEK kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa madreva wote wa naoendesha vitu vya moto
, wanajamii ,na wamiliki wa vitu vya moto
kwa lengo la kuweza kupunguza ajili
za barabarani.
Mjema alisema kutokana na tafiti zilizofanywa
na jeshi la polisi wamegundua
kuwa ajili nyingi zinazotokea
barabara zinasababishwa na
madreva kupuuzia sheria za barabarani na
alama za barabarani.
Pia alisema mbali na sababu hizo kuna sababu niyngine kama za ubovu wa miundo
mbinu na ubovu ya vifaa vya moto ambazo
hutokea mala chache sana lakini alaisema ajali nyingi husababishwa na
madreva kwa kuto kuzingatia sheria
na taratibu za barabarani.
Desdery Kyayonka mkufunzi katika semina
hiyo alisema mada zitakavyo
fundishwa ni sheria za usalama barabarani, alama za usalama barabarani,
ujasilia mali, na dhana ya pilisi jamii kwa muda wa siku saba.
Kayonka alisema kumekuwako na mwitikio mdogo wa wa watu wanao endesha vitu vya moto hasa wanaoendesha pikipiki za magurudumu
mawili bodaboda kuhudhuria mafunzo
hayo kitu alichowataka kuhudhuria
mafunzo hayo ambayo alisema yanafaida kubwa sana kwao na kuwarahisishia
upatikanaji wa leseni za udreva.
K wa upande wake askari wa
usalama barabarani wilyani hapa Novaty
Magoma alisema watapisha msako mkali kwa madreva wote
wasiokuwa na leseni na wanaendesha vitu vya moto na hawajahudhuria mafunzo hayo .
Magoma alitumia fursa hiyo kuwataka madreva wote wa bodaboda kutii sheria bila shuruti na
kupunguza misaha ambayo inaghalimu
maisha wa watu na mali zao hivyo
alimewataka madreva wote kuhudhuria mafunzo hayo.
Mmoja wa wanasemina hiyo Letisia
Mwenda alisema pamoja na kuwapo kwa mafunzo hayo
yatawajengea uwezo wa kuelewa sheria ambazo baadhi ya maaskari wamekuwa wakitumia mmuanya wa
huo kuwanyanyasa na kuwageuza
baadhi ya waendesha bodaboda kama mitaji yao ya kujipatia kipato chao cha kila siku.
Pia Letisia amewataka madreva
wenzake kuweza kuhudhuria mafunzo hayo ambayo alisema kuwa yanamanufaa
makubwa kwa ajili ya maisha yao na mali
zao na mali za matajili wao.
Comments
Post a Comment