KILIMO CHA UMWAGILIAJI HATARINI KUTOWEKA CHAMKOLOMA-KISA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.
N a Stephen noel – Kongwa.
KILIMO Cha umwagiliaji
katika kata ya chamkoloma wilyani Kogwa kipo hataririni kutoweka na kufutika kabisa kutokana na uharibifu
mkubwa wa mazingira unaoendelea katika vijiji vya Tubugwe juu, Mseta,Kiboriani, na kijiji cha
Sagala.
Ras fm imetembelea
maeneo hayo ambayo ambayo ni Tubugwe kibaoni, tubugwe juu,mseta A, Mseta
bondeni,chamkoloma, makole na ambapo ilijionea uharibifu mkubwa wa mazingira
,ikiwemo wanachi wa vijiji hivyo kukata miti sana katika milima hiyo na kulima katika vyanzo vya maji, ambayo imekua ni tishio kubwa kwa baadhi ya mabonde kuanza kukausha maji na
kupungua kwa uzalishaji wa mazao kama
miwa na maharage yanayo limwa katika mabonde hayo.
Mtendaji kata ya chamkolama
Bwana Fanuel Ng’anda alisema kata hiyo
ambayo imekuwa ni tegemeo kubwa la mazao ya mbogamboga ambayo hulisha karibu mkoa mzima wa
Dodoma na mkoa jirani kama morogoro ambayo alisema kwa sasa imepungua
sana.
Aidha alisema siku hadi siku zinavyo zidi kusonga mbele tatizo
linazidi kuwa kubwa na maji yanazidi kupungua na kutishia kukauka
kwa vyanzo vya maji ambavyo ndivo
tegemeo kubwa la maisha ya watu wa kata hiyo.
Hatahivyo
alisema kuna baadhi ya wanasiasa
wamekuwa kikwazo katika kulifanikisha
suala hilo ambalo alisema ni kuwakingia vifua waharibifu wa mazingira kwa madai
ya kupoteza kura hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika kipindi cha uchaguzi October mwaka huu.
Kwa upande wake A mos Leganga
mwenyekiti wa mradi wa maji mesema kuwa kutokana na shughuli
kubwa za kibinadamu kufanyika katika milima ya hifadhi, kulima katika
vyanzo ya maji kunatishia uendelevu wa
upatikanaji wa nmaji safi katika vijiji hivyo.
Pia alisema kumekuwako na
changamoto kubwa ya viongozi wa wilaya
ya mpwapwa na wilaya ya kongwa kushidwa kuafikiana juu ya mbinu zitakazo nusuru mlima wa
kiboriani ambao ndio chazo kikubwa cha
upatikanaji wa , maji katika wilaya hizo
kwa sababu alizo ziita kuwa ni za wanasiasa kuwalinda waharibifu wa
mazingira.
Hata hivyo alisema milima hiyo imeanza
kuonyesha uhafadhali baada ya
kukabidhiwa kwa wakala wa misitu
kusimamia, tofauti na hapo awali
ambapo milima hiyo ilikuwa inasimamiwa na serikali za vijiji ambazo
zimeonyesha kushidwa kutatua tatizo
hilo.
Diwani wa kata ya chamkoloma Daimon Mdumbe
alikanusha kwa baadhi yawanasiasa wakiwemo madiwani kuhusika katika
kuwakingia vifua waharibifu wa mazingira kwa kile alicho kisema kuwa, maisha ni zaidi ya kura wanazo zipata hivyo aliwataka watendaji wote wa serikali kufuata sheria na
taratibu za kazi kuwaadhibu
waharifu wa mazingira.
Aliongeza kuwa milima wa
Kiboriani ambao ndio mlima mkubwa ambao
upo katika hifadhi za milima za tao ya mashariki
lakini umehribiwa sana kitu alicho
kisema kuwa wamepanga kukaa kikao cha pamoja
na uongozi wa wilaya ya mpwapwa pamoja na kongwa ili kuweza kutafuta
njia ya pamoja ya kulitatua tatizo hilo.
Ikumbukwe kuwa katika katiba ya
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 katika sehemu ya tatu juu yahaki na wajibu kifungu cha 27
kinachodai kila mtu ana haki ya kulinda
mali asilia sambamba na sheria ya kulinda mali ya umma ya mwaka 1984 namba 5 ibara 6 hivyo anaye
haribu mazingira anakinzana na katiba hii.
Comments
Post a Comment