WALIMU WAUNGA MKONO MGOMO KWA ALMIA 98.4 MPWAPWA
Na noel Stephen mpwapwa
30 julai 2012
Asilimia 98.4 ya walimu wote wa wilaya ya mpwapwa waunga mkono mgomo wa walimu unaoendelea kote nchini wakati asilimia 1.6 hawakubaliani na mgomo huo.
Ni kauli iliyo tolewa na mwenyekiti wa chama cha walimu wilayani mpwapwa Bi NELEA NYANGUYE mkoani dodoma alipokuwaakiongea na waandishi wa habari ofisi kwake juu ya kutoa msimo wa chama hicho juu mgomo wa walimu wote katika wilaya ya mpwapwa.
Bi nyanguye alisema kufuatia kauli ilioyo tolewa na Raisi wa chama hicho taifa wilaya ya mpwapwa imeunga mkono kwa asilimia 98.4 mgomo huo kwa kuishinikiza serikali kuwalipa haki zao za msingi kama watumishi wa serikali .
Aidha bi Nyanguye alisema kuwa kufuatia kifungu cha 80 kipengele kidogo cha (1)d cha sheria ya mahusiano kazini ya mwaka 2004 walimu ambao ni wanachama wa CWT walianza zoezi la kupiga kura tarehe 25 julai 2012 na kumalizika tarehe 27julai na na asilimia 98.4 ya walimu wote wa wilaya ya mpwapwa waliunga mkono mgomo huo.
Alisema wilaya ya mpwapwa ina walimu 1491 ambao waliunga mkono ni walimu 1470 ambapo alisema kuwa walimu 21 hawakuunga mkono mgomo huo.
Na alidakuwa mgomo huo unahusuisha walimu wa shule za msingi, sewkondari, vyuo vya ualimu ,na chuo cha maendeleo ya jamii (FDC)
Kwa upande wake afisa elimu wa wilaya hiyo bwana Musa Singo siku siku ya ya mgomo alikuwa akitembelea mashuleni akiwa ameambatana na afisa elimu taaluma sekondari na Afisa Elimu taluma msingi wakiwa wakiwataka wallimu walio fika shuleni hapo na kupiga sogo ofisini kuwataka waingie madarasani na kufundusha huku akiwajazisha fomu ya mgomo kwa walimu walio kuuwepo katika shule hizo .
Bwana Singo akitakiwa kuelezea mgomo huo kwa waandishi wa habari aligoma kulisema hili na kuwataka waandishi wa hanbari kwenda kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule msingi chgazungwa ambapo ndipo alipokutwa na wandishi wa habari akiwashawishi walimu kuachana na mgomo huo .
Kwa upande wa afisa elimu huyo na kuingia madarasani na kuanza kufundiisha japo kwa kwa shingo uypande lakini wengine waliendelea na msimamao wao wa kukaa ofisini na kuendelea kupiga sogo
K atika shule nyingi hapa mpwapwa zilionekana kuto kuwa na walimu wakati walimu wengi wakiwa wamesaini katika kaitabu cha mahudhurio ya kila siku lakini hawakuwepo madarasni .
Na pia imeadhili zoezi zima la wanafunzi ambao walitakiwa kuanza mitihani ya kufungia shule lakini wanafunzi wengi walionekana wakilandalanda kwenye viunga vya shule hizo bila kujua muelekeo wao..
Comments
Post a Comment