mpango wa serkali waleta nafuu kwa wafugaji kenya

rikali unaotoa mifugo kwa familia zilizopoteza wanyama wao wakati wa ukamu wa mwaka jana.
  • Msichana akichunga mbuzi wake kaskazini ya Nairobi. Serikali ya Kenya imenunua mifugo kwa wachungaji ili kuwasaidia wale walioathirika na ukame. [Na Tony Karumba/AFP] Msichana akichunga mbuzi wake kaskazini ya Nairobi. Serikali ya Kenya imenunua mifugo kwa wachungaji ili kuwasaidia wale walioathirika na ukame. [Na Tony Karumba/AFP]
Kwa mujibu wa mafisa wa serikali, familia 79,041 zilisaidiwa kupitia mpango huu, uliomalizika mapema mwezi huu. Waliofaidika nao waliiambia Sabahi kuwa mpango huo utawasaidia kuanza upya maisha yao.
Fatuma Ali Hassan, mkazi wa Wilaya ya Wajir mwenye umri wa miaka 52, alisema familia yake ya watu wasita iliporomoka baada ya kupoteza ng'ombe wake 87 kutokana na ukame. "Tulikwishapoteza matumaini yote baada ya kupoteza chanzo chetu pekee cha kutupatia riziki mpaka pale serikali ilipotangaza hatua za kuingilia kati," aliiambia Sababhi.
Baada ya kupoteza wanyama wake, alitegemea chakula cha msaada kutoka kwa serikali na mashirika ya msaada kama suluhisho la muda mfupi. Hassan alisema alikuwa na bahati ya kuwa miongoni mwa familia waliofaidika na mpango wa seriklai katika kijiji cha Khorof Harar village. Alipata mbuzi 10.
Sabdow Ahmed Musa, mwenye umri wa miaka 42 na aliyefaidika kutoka Wilaya ya Wajir, aliiambia Sabahi hakutarajia katu kurejea teana katika maisha yake ya uchungaji baada ya ng'ombe wake 102 kufariki.
Baba huyo wa watoto watano alisema kuwa wakati wanyama wake waliĆ²fariki, waliachwa bila ya chochote. "Ninaishukuru serikali kwa kunipa ngombe watatu na mbuzi saba. Kwa mapenzi ya Mungu, nitaanza upya kutoka hapa," alisema.
"Bila ya msaada huu, baadhi yetu tulibakia kuombaomba na kupanga foleni katika vituo vya ugawaji wa chakula cha msaada, ambapo chakula kilikuwa hakitoshi kutulisha sote. Sasa tuna matumaini ya kunyanyuka tukiwa tunajitegema,"
Ali Mohammed Jehow, msaidizi wa utawala katika eneo la Arbaqeramso, Wilaya ya Wajiri, aliiambia sababhi kuwa mpango huo ulitoa kipaumbele kwa familia zilizoathirika zaidi, kama zile zinazoongozwa na mama wajane au wale wanaowatunza watu walemavu au watoto yatima.
"Kamati ndogo imeundwa katika kila kijiji ili kuamua jinsi ya kuwalenga wale walioathirika zaidi na wako katika hatari, na jinsi ya kunufaika [kutokana na mpango huu]. Orodha ya watakaofaidika baadaye ilithibitishwa na maafisa wilaya wa maendeleo ya mifugo ," Jehow alisema.
Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mifugo Mkoa wa Kasazini Mashariki Gideon Wambua aliiambia Sabahi kuwa serikali ilitumia shilingi milioni 60.5 (dola 720,000) kununua mifugo kutoka kwa wachungaji wengine.
Alisema serikali ilinunu ng'ombe, mbuzi, kondoo na ngamia 20,579 na

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.