AL-SHABABU WAUWANA WENYEWE KWA WENYEWE KUOGOPA KUSALITIANA

a serikali za kigeni kunaonyesha ukosefu wa imani ndani ya vyeo vya kikundi cha wapiganaji, wachambuzi wa kisiasa na waangalizi wanasema
  • Mpiganaji wa al-Shabaab amesimama akilinda wakati mamia ya wakazi wakiangalia adhabu ya kukatwa viungo hadharani. Al-Shabaab hivi karibuni iliwaua wanachama wake watatu kwa tuhuma za kupeleleza kwa niaba ya serikali za kigeni. [Mustafa Abdi/AFP] Mpiganaji wa al-Shabaab amesimama akilinda wakati mamia ya wakazi wakiangalia adhabu ya kukatwa viungo hadharani. Al-Shabaab hivi karibuni iliwaua wanachama wake watatu kwa tuhuma za kupeleleza kwa niaba ya serikali za kigeni. [Mustafa Abdi/AFP]
Al-Shabaab ilisema watu watatu -- Ishaq Omar Hassan,miaka 22, Yasin Osman Ahmed,miaka 23, na Mukhtar Ibrahim Sheikh, miaka 33 -- walikuwa wanapeleleza kwa ajili ya Shirika la Upelelezi la Marekani na Shirika la Upelelezi la Uingereza MI6.
"Hassan na Ahmed wote wawili walihusika na vifo vya Bilal al-Berjawi na wengine watatu [wanachama wa al-Shabaab]," shirika hilo linalohusiana na al-Qaeda lilisema katika mtandao wake wa Twitter tarehe 22 Julai. "Wawili hao waliweka vifaa vya ufuatiliaji katika magari ya al-Berjawi & kaka zake ambayo waliyaongoza makombora yaliyoshambulia vitongoji vya Mogadishu."
Al-Berjawi, mwenye uraia wa nchi mbili za Lebanon na Uingereza ambaye alivuliwa uraia wa Uingereza, aliuawa katika shambulio la kombora mwezi Januari nje ya Mogadishu. Iliripotiwa kuwa alikuwa kamanda msaidizi wa al-Qaeda nchini Somalia.
Waliyoshuhudia huko Marka walisema watu hao watatu waliuawa na kikosi chenye silaha katikati ya mji.
"Wapiganaji wa al-Shabaab ilitumia vipaza sauti vilivyofungwa katika malori kuwaita watu kushuhudia mauaji na watu walipokusanyika uwanjani, dazani ya wapiganaji waliyofunika nyuso zao waliwafunga vitambaa machoni watu hao watatu na kisha kuwapiga risasi, wakiwaua hapo hapo," mkaazi wa Marka Mohamed Said, miaka 34, aliiambia Sabahi

Tatizo la Al-Shabaab la kujiamini.

Omar Dahir, mkurugenzi wa Kituo kilichopo Mogadishu cha Marekebisho na Mjadala, alisema matatizo ya al-Shabaab yanatokana na kuongezeka kwa mgawanyiko miongoni mwa wanachama na kunaweza kusababisha kusambaratika kwa haraka kwa kikundi katika siku karibu zijazo.
"Kuna kutojiamini ndani ya al-Shabaab, kwa kuwa kikundi hakiwaamini wanachama wake na sasa viongozi wake hawaaminiani," Dahir aliiambia Sabahi. "Uamuzi wa al-Shabaab kuwaua wanachama wake watatu huko Marka unaonyesha ukosefu wa imani ambao unakikabili kikundi."
"Hii inaweza kuwa mwanzo wa kuvunjika kwa mipango ya mapigano iliyoandaliwa ndani ya kundi hilo, ambalo tayari linasumbuliwa na mgawanyo mkubwa," Dahir alisema.
Alisema al-Shabaab inaweza kukimbilia kuwaua kwa siri wengi wa wanachama wake kwa kuogopa kuwa kufanya mauaji mara mingi mbele ya wananchi kunaweza kuyumbisha umoja wa kundi hilo.
"Kundi hili litamuua mwanachama yeyote anyeshukiwa kuwa na uhusiano na pande za nje kwa sababu wanaogopa kuwa mashirika ya upelelezi ya Ulaya yanaweza kupenyeza kwenye kundi hilo na kuwalenga viongozi wao wanaotakiwa," Dahir said.
Al-Shabaab ilisema katika mtandao wa Twitter kuwa imezindua kampeni kubwa ya kukabili upelelezi ili kusafisha nchi kutokanana na majasusi hao .
Mwaka uliopita , kiongozi wa al-Shabaab Mualim Hashi Mohamed Farah alisema Kitengo cha upelelezi cha Ulaya kimepenyeza kwenye safu ya maaskari wa al-Shabaab, na mawakala wa pande mbili wanaojifanya kuwa wapigananaji wa vita vitakatifu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.