TAMBO ZA UDIWANI ZASHIKA KASI KATA YA MPWAPWA MJINI
Na noel Stephen Mpwapwa
WiTo umetolewa kwa wananchi wote wilayani mpwapwa mkoa wa Dodoma kuweza kumchagua mtu kutokana na sera zake na chama chake bali kuachana na hatua za kumchagua mtu kwa kufuata mazoe ya chama .
WiTO huo umetolewa na Katibu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA FABIAN MOKE alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana juu kichanag`anyilo cha udiwani kata ya mpwapwa mjini utakao fanyika sept 30 mwaka huu.
MOKE alisema kuwa kuna mazoea ya wananchi ya kuchagua mtu kwa sababu anatoka kwenye chama Fulani bila kupima uwezo wake wa kujieleza kujenga hoja na kuweza kuwatetea wanachi wanyonge wanaokandamizwa na utawala wa chama TAWALA.
Aidha moke alidai kuwa kwa wilaya ya mpwapwa nzima hakuna diwani wa chama cha upinzani ndio maana madiwani wa chama hicho kuweza kubuluzwa na watendaji wa Halmashauri hiyo na kusahau kazi yao ya kuwatetea wananchi,na halmashauri hiyo kuendelea kutumia pesa ya mlipa kodi mnyonge bila kuhoji na kupelekea halmashuri hiyo kupata hati ya mashaka juu matumizi ya pesa za halmashauri hiyo kwa 2011/2012.
Uchaguzi huo ambao ni uchaguzi mdogo uanakuja kufuatia aliye kuwa diwani wakata hiyo kufariki dunia april 7mwaka huu na kuiacha kata hiyo bila kuwa na diwani yeyote.
Pia alisema kuwa Chadema wamejipanga kuchukua jimbo la mpwapwa mjini kwa sababu wameona ndani ya halmashauri hiyo kukiwa na madiwani wa vyama tofauti watendaji wa halmashauri watafanya kazi kwa bidii na wananchi kushindwa kunyonywa kwani chadema “tunataka maendeleo kwa wananchi na sio kuwanyonya wananchi.”alisema MOKE
Alisema kuwa chama chake kitamteuwa mgombea atakaye peperusha bendera ya chadema na kuwanufaisha wananchi kimaendeleo na sio kuendelea kukaa na chama kimoja lazima wanampwapwa waamke na sio kuwa katika hali ya chama kimoja
Na aliongeza kuwampaka sasa kuna wanachma wanne walio onyesha nia ya kuingia katika kinyang`anyilo cha udiwani septemba mwaka huu.
“Katika chama chetu hakuna mgogoro wowote ndani ya chama wala makundi hapa ni kazi za kimaendeleo na hasa kwa kuwaletea wananchi manufaa zaidi, napenda kusema wananchi wa mpwapwa wanaipenda sana chadema na kuikubali kuwa wakichukuwa udiwani kata ya mpwapwa mjini hali itabadilika itakuwa mpwapwa nyingine sio ya sasa”,alisema
Alimalizia kuwa wananchi wa mpwapwani lazima wajitokeze kwa wingi kwenye kampeni ili kuwajua wagombea na kujua sera zao za chama na kumjua mtu binafsi ili siku ya kupinga kura wachague mtu wanaempenda wao wananchi wa mpwapwa mjini.
Comments
Post a Comment