WASTAFU WALIA KUKOSA UMOJA
Katibu wa chama cha walimu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma bwana Pankras Ngamesha ameiomba serikali ya awamu ya tano kuwachukulia hatua waajili wanaozembea kuwasilisha michango ya makato katika mifuko ya pesheni hapa nchini Ngamesha alitoa kauli hiyo alipokuwa akiongea katika hafla ya kuwashika mkono wa pongezi walimu 34 wa wilaya ya mpwapwa mkoa wa Dodoma walio stafu utumishi wao mwezi march na mwezi mei mwaka 2016. Ngamesha alisema kumekuwako na chanagamoto kubwa kwa wastafau kuishi maisha magumu mala baada ya kumaliza utumishi wao serikali kutokana na kucheleweshewa mafaoa yao kutoka katika mifuko ya hifadhi ya jamii (PSPF). Aidha Ngamesha aliwakabidhi bati 20 kila mmoja walimu kumi waliostafu ambao walikuwa wanachama wa chama cha walimu hapa wilayani kama kuwashika mkono wa kwaheri na kutambua mchango wao wa kukutumikia chama hicho na serikali kwa ujumla . ...