WAKAZI WA KIBAKWE WAPATA CHUMBA CHA UPASUAJI.
wakazi wa kibakwe
WAKAZI 82,703
wa tarafa ya Kibakwe wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma watanufaika na huduma za upasuaji mala baada ya kukamilika kwa chumba cha
upasuaji katika kituo cha afya cha
tarafa hiyo.
Kwa mujibu wa mganga mkuu wa wilya Dkt ,Said Mawji amesema kuwa chumba hicho cha upasuaji ni moja wapo ya miradi ya maendeleo ya afya
iliyo anza kutekelezwa katika katika mwaka wa fedha wa 2013/2014.
Mawji alisema mala bada ya kukamilika kwa
chumba hicho kitasaidia wagojwa wa tarafa hiyo waliokuwa wakipewa rufaa kwenda
kufanyiwa upasujai katika hospitali ya
wilaya na kupunguza usumbufu kwa wagonjwa na kuokoa maisha ya akina mama
na watoto.
Aidha Dkt Mawji alisema jengo hilo japo kuwa lilikamilika muda mrefu
lakini halikunza kutumika kutokana na
ushauri wa kitaalamkutoka ka timu ya uendeshaji wa shughuli za afya mkoa
RHMT na timu ya uendeshaji ya
wilaya CHMT kuwa lengo hilo lilikuwa na
mapungufu makubwa kabla ya kuanza
kutumika.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa
halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa Mohamed Maje alidai jengo hilo limegharimu jumla ya shilingi
milion 59,514,299/=ambazo ni michango
mfuko wa wa afya (MMAM)pamoja na mchnago wa fedha kutoka bima ya afya iliyo
boreshwa CHF.
Maje alisema kwa sasa chumba hicho kimekamilika na mwanzoni mwa mwezi septemba itaanza kutumika na kuwawezesha wakazi wa
tarafa ya kibakwe kuweza kupata huduma hizo kirahisi na karibu zaidi.
Hata hivyo Maje alisema ujenzi wa chumba cha upasujai ni miongoni mwa
utekelezaji wa sera ya afya ya kuwa na kituo cha afya kila tarafa na kuwa na
chumba cha upasujai .
Comments
Post a Comment