TASAF YAONYESHA MAFANIKIO KWA WALEGWA MPWAPWA
BAADHI ya WANUFAIKA wa
mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma , ikiwa ni miaka miwili tu tangu
mpango wa uhuwirishaji fedha kwa kaya maskini wanufaika yashuhudia njisi ulivyo weza
kubalisha maisha yao kutoka hali za chini kwenda hali za unafuu wa maisha.
Mmmoja wa wanufaika wa mapango huo kutoka katika kijiji cha ikuyu
kata Luhudwa Bi Anna Mduwile alisema kuwa alisema kabla ya mpango huo haujanza
kutekelezwa alikuwa hana makazi ambapo ilikuwa inamlazimu kulala kwenye chumba
kimoja na watoto wake wanne pamoja na baba yao .
Aidha Bi Anna alisema
kwamba baada ya mpango huo
kuanzishwa alijitahidi kujenga nyumba ya bati 16 yenye
vyumba viwili na sebure na
kufuga mbuzi ambapo alisema mpaka sasa tangu anze kufuga amefikisha mbuzi 4 mbao wanasaidia kuinua kipato cha familia yao.
Wakati huo huo wanufaika wa mradi huo katika kijiji cha
bumira wamedai kuwa baadhi ya wanufaika
wa wa mradi huo kwa watu wenye umri
mkubwa pesa hizo wamekuwa wakizitumia
kununulia maji ya matumizi ya nyumbani
kutokana na uhaba wa maji unao kikabili kijiji hicho.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya jamii ya usimamizi wa mpango
huo bwana Lugano Samsoni alisema kuwa katika kijiji hicho dumu moja
la maji huunzwa kwa shilingi 700 hadi
1000 ambapo kaya moja inahitji madumu
4hadi 5 kwa siku , kitu alicho kisema
kinashidwa kuwanufaisha wazee walio ktika mpango huo.
Hata hivyo mwezeshaji
wa mpango huo ngazi ya wilaya bi Hilda Mgomapayo alidhibitisha mpango huo kuweza kuinuia
kiwango cha maisha kwa wanafaika kwa
kuboresha makazi, kubuni biasahara ndogondogo, na kuwasidia watoto wanao soma
kuwanunulia mahitaji yao bila shida.
Bi Mgomapayo
alisema”Kiukweli mpango huu umeweza kuonyesha mafanikio mazuri sana umeongeza
idadi ya akina mama wanaojifungulia katika mikono salama , imepunguza utoro wa
watoto shuleni kutokana na mlegwa asipo timiza masaharti hayo pesa yake hukatwa
hivyo hawakubali pesa ikatwe kwa hiyo wanajitahidi kuzingatia masharti”alisema Mgomapayo.
Kwa upande wake kaimu mratibu wa TASSAF wilayani hapa Paskal
Jeremia alisema kuwa katika kipindi cha mwezi wa julai na Agosti jumla tsh
210,795,454.55/=zimepokelewa kuwezesha zoezi ngazi ya wilaya na jumla ya wakazi 6256 wamenufaika.
Paskal ametumia fursa hiyo kuwahadhalisha baadhi ya walegwa wanaopokea pesa na
kuzitumia kwa kinyume cha makusudi
ikiwamo kulewea pombe kitu alichosema wataweza kuondolewa katika mpango huo na kuwaingiza wahitaji wengine.
Comments
Post a Comment